Top Stories

Rooney amuunga mkono Kane kuivunja rekodi yake.

Harry Kane ana nafasi ya kuwa mfungaji bora wa taifa la England na hilo ni kwa mujibu wa Wayne Rooney. Rooney amempa moyo Nahodha huyo wa England Kwamba anaweza kufikia magoli 53 ambayo ameyafunga yeye akiwa na taifa hilo. Rooney mshambuliaji wa zamani wa Everton na Manchester United amestaafu rasmi kulitumikia taifa la England baada ya kucheza mechi ya mwisho Alhamis usiku katika uwanja wa Wembley England ikishinda 3-0 dhidi ya Marekani. Baada ya Rooney kustaafu akiwa Ndio kinara wa magoli katika taifa la England akicheka na nyavu mara 53…

Read More

Vita ya Dernmak na Wales Kesho Bale yutayari kuwanyoosha.

Kocha wa timu ya taifa ya Wales Ryan Giggs ameweka wazi Kwamba Gareth Bale yuko fiti kuivaa Denmark kwenye michuano ya UEFA NATIONS LIGUE mchezo wa kamua hatima ya Kundi lao Kesho. Bale alikuwa matatani kuwepo katika mchezo huo wa Kesho kutokana na jeraha alilolipata siku ya jumapili wakati Madrid ikiichapa 4-2 Celta Vigo. Bale (29) alijunga na kikosi cha Wales leo asubuhi na Giggs ana matumaini yakumtumia katika mchezo wa Ijumaa hii dhidi ya Denmark utakaofanyika mjini Cardiff. “Anaonekana yupo sawa wiki hii na yupo tayari” maneno ya Giggs…

Read More

Leo mpaka Dec 15 harakati za Usajili zimeanza rasmi.

Jana Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kupitia Mtendaji wake Mkuu Boniface Wambura, ilithibitisha kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili leo Alhamisi Novemba 15 2018. Wambura alisema kulingana na kalenda ya mashindano, dirisha la usajili limefunguliwa leo na litafungwa Disemba 15. Tofauti na miaka ya nyuma ambapo ligi ilikuwa ikisimama kipindi chote cha usajili wa dirisha dogo, mwaka huu ligi itaendelea. “Ni kweli kwa kalenda ya mashindano November 15 hadi December 15 linafunguliwa dirisha dogo la usajili lakini ukiangalia ratiba yetu ligi haitasimama kupisha dirisha dogo la usajili,” alisema Wambura “Ligi…

Read More

Katibu mkuu wa zamani Yanga aingia kupambania Uenyekiti Jangwani.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, amechukua fomu ya kugombea Uenyekiti ndani ya klabu hiyo jana. Tiboroha amefikia maamuzi hayo akiamini anaweza kuwa chachu ya mabadiliko ndani ya Yanga na kuamua kuchukua fomu hiyo. Mwanachamu huyo ambaye aliwahi kuwa kiongozi ndani ya Yanga miaka kadhaa nyuma na baadaye kuelekea Stand United, amekuwa mtu pekee aliyechukua fomu hiyo. Halikadhalika katika upande wa Makamu Mwenyekiti, Yono Kevela naye amechukua fomu hiyo. Kwa upande wa Wajumbe waliochukua fomu ni pamoja na Hamad Ally, Benjamin Jackson, Silvestoer Haule, Musa Katabaro,Said Baraka, Pindu Luhoyo,…

Read More

Modric hana huruma Sasa awaburuta tena Ronaldo na Salah na kutwaa tuzo hii.

Kiungo Luka Modric amezungumzia Furaha yake baada ya kutwaa tuzo ya Goal 50 mwaka 2018 ambayo inapewa kwa mchezaji Bora ndani ya miezi 12 na akasema Madrid wamejipanga kutwaa UEFA Champions League kwa msimu wa nne mfululizo. Mcroatia huyo amekuwa na mwaka wa mafanikio baada ya kubeba taji la UEFA Champions League akiwa na Klabu yake pamoja na kufika fainali ya michuano ya kombe la Dunia pale Russia akiwa na taifa lake. Na hii imemsaidia kujikuta akipata tuzo za juu kama mchezaji, tuzo ambazo ni Mchezaji Bora wa FIFA wa…

Read More

Trippier aondoshwa kikosi cha Taifa aungana na Welbeck Kujiuguza.

Mlinzi wa pembeni wa klabu ya Tottenham Kieran Trippier ameondoshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kilichoitwa kwa ajili ya michezo inayofuata dhidi ya Marekani na Croatia. Trippier alipata majeraha kwenye mchezo wa klabu yake ikishinda 1-0 dhidi ya Crystal Palace siku ya jumamosi na ndiyo sababu ya kumchomoa kwenye kikosi cha (Simba watatu). Alifanikiwa kuwasili katika kambi ya timu ya taifa siku ya jumatatu iliyopo  kwenye viunga vya St.George’s Park siku ya jumatatu lakini akarudishwa kwenye klabu yake. Mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck ni mchezaji mwengine pekee…

Read More

Ustaarabu wa wachezaji kutoka Barca kwenda Darajani huwenda ukamkuta huyu kijana.

Chelsea wanataka kupeleka ofa ndani ya klabu ya Barcelona kwa ajili ya kupata saini ya kiungo Denis Suarez ambapo kocha wa The Blues Maurizio Sarri anataka kujaribu kumsajili tena baada ya kumkosa alipokuwa kocha wa Napoli. Suarez hajagusa kabisa mpira msimu huu katika LA LIGA akiwa hajapewa kabisa nafasi hiyo Kocha isipokuwa labda tu kwenye michuano ya Copa Del Rey. Sarri anamkubali sana Suarez na alijaribu kumsajili alipokuwa Italia na Suarez ameonesha nia ya kutaka kuondoka Barca baada ya kushindwa kupata nafasi kikosi cha Ernesto Valverde Suarez amefunga magoli 6…

Read More

WALAZIMIKA KUTEMBEA KWA MGUU KWENDA KAZINI, NI BAADA YA MAGARI YA ABIRIA KUGOMA

Mamilioni ya wasafiri kote nchini Kenya leo wamelazimika kutembea kwa mwendo mrefu hadi sehemu zao za kazi ama kutumia njia mbadala za usafiri baada ya magari ya uchukuzi wa umma ya matatu au daladala kususia kuhudumu. Wamiliki wa matatu wanapinga hatua ya serikali kutekeleza sheria kali za kudhibiti usalama wa abiria. Sheria hii inawataka wamiliki wa matatu waweke mikanda ya usalama, vidhibiti mwendo vya kidijitali na magari yote yawe na dereva na wahudumu walioajiriwa.

Read More

Mourinho “hatushuki dararaja”.

Kipigo walichokipokea Manchester United Jana kutoka kwa jirani zao Man City kinaifanya United kuwa karibu na nafasi mbaya katika msimamo wa ligi kuu ya England lakini Jose Mourinho hana shaka na hilo. Manchester United baada ya mechi ya jana wanakalia nafasi ya 8 wakiwa na alama 20 ukiwa ni utofauti wa alama 12 kati yake na kinara Manchester City. Hali hiyo ya kimsimamo inafanya wachambuzi kumtupia vijembe Mourinho wakimuuliza haoni Kwamba atashuka daraja, lakini Mwenyewe Mourinho kajibu “sifikiri kama tutashuka daraja” “Timu moja imeanza vizuri msimu ikiwa na nguvu wakati…

Read More