Breaking News: Baba Mzazi wa Mbunge Profesa Jay Afariki dunia.

Habari zilizotufikia hivi punde Kutoka Mikumi ni kuhusiana na Kifo cha Baba yake na Mbunge wa jimbo la Mikumi kupitia Chadema, Joseph Haule Maarufu kama Profesa jay ambacho kimetokea katika hospitali ya St Kizito iliyopo Mikumi Mkoani Morogoro. Profesa jay amethibitisha Taarifa hizo kwa  njia ya Simu, akiwa Jijini Dodoma katika vikao vya Bunge vinavyoendelea.        

Read More

Aliyemuita Rais UHURU KENYATTA na Wakenya Wote kuwa ni “Ngedere” amekumbana na Hiki, Ubalozi wa China umetoa Kauli !!

NCHI ya Kenya imeamua kuchukua maamuzi mazito dhidi ya Mfanyabiashara mwenye asili ya China, anayetambulika kwa jina la LIU JIAQI ikiwa ni baada ya kutoa kauli ya ubaguzi na Lugha chafu kwa Wananchi wa Kenya pamoja na Rais wa Nchi Hiyo, Uhuru Kenyatta. Taarifa ambazo zilisambaa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii zikimuonesha mfanya biashara huyo wa Piki Piki akiwaita wakenya wote kuwa ni “Ngedere” sanjari na kumtaja Rais Uhuru Kenyatta pia kuwa ni “ngedere” ziliifanya Idara ya Uhamiaji nchini humo kuchukua jukumu la kumuondoa haraka iwezekanavyo Lui Jiaqi nchini…

Read More

BOBI WINE- “Kuna Waganda Wengi Gerezani Wanaopitia Mateso Kama Niliyoyapata”

MSANII Bobi Wine (Jina Kamili- Robert Kyagulanyi ) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kyaddondo Mashariki Nchini Uganda, hatimaye alipata nafasi ya kuzungumza hadharani baada ya “sintofahamu” yake na Serikali ya Nchi ya Uganda. Kama utakuwa unakumbuka vizuri, Bobi Wine aliingia katika Mtafaruku mkubwa na Vyombo vya Usalama pamoja na Serikali kiujumla kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kuanzishwa kwa vurugu na wafuasi wake katika kampeni za Uchaguzi Mdogo Nchini humo, hali iliyopelekewa kukamatwa na kuzuka kwa maandamando ya Wafuasi wake dhidi ya Serikali wakitaka awe Huru Katika hali…

Read More