Mbona mtu akifia kitandani anafanya mapenzi hamchomi kitanda?

Hoja mbalimbali zinaendelea kutolewa na Wabunge pale Dodoma katika mkutano wa Bunge na hoja hizo kupatiwa majibu na mawaziri wanaosimamia wizara husika moja Kati ya hoja iliyoibuliwa bungeni ni kutoka kwa Mbunge wa Konde Khatibu Saidi Haji Kuhusu maabusu kufia mikononi mwa polisi.

Mbunge Khatibu Saidi alikuwa akimlenga Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola atoe majibu akimweleza hata siku za Karibuni wananchi wamekuwa wakisusia kuzika maiti za watu wanaofia katika vituo vya polisi.

 

 

Waziri Lugola 

Waziri Lugola kwa upande wake kwanza amekemea tabia ya wananchi kuchukua maamuzi ya kuvamia vituo vya polisi na kuchoma moto na kuwaambia wananchi mtu anfia popote pale na kuhoji mbona anayekufa akifanya mapenzi watu hawaendi kuchoma kitanda na nyumba kwamba amefia mikononi mwa kitanda. 

 

Related posts