Vettel “adui anaenibania kushinda Formula One”

Dereva wa timu ya Ferrari Sebastian Vettel amejiita “Adui mkubwa” katika harakati za kupambania taji la Formula One dhidi ya Lewis Hamilton wa Mercedes.

Vettel wikendi hii atakuwa katika vita ya kushindana katika mashindano ya Singapore Gp huku akiwa na mzigo wa kupunguza point 30 alizopitwa na mpinzani wake Lewis Hamilton wa Mercedes katika msimamo wa madereva. 

     Sebastian Vettel katika jezi ya Ferrari 

Inaeleweka Ferrari wana magari ya kasi kuliko Mercedes na wanapewa nafasi ya kushinda wikendi hii na Vettel anaamini wana nafasi kubwa ya kuwa Mabingwa msimu huu.

“Mambo yamenyooka kwa upande wangu naamini mimi binafsi ndio adui mkubwa” Vettel alijibu alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kupoteza point zaidi mbele ya Lewis Hamilton.

Kwa upande wa Hamilton amejinasibu kuwa makini katika mbio zilizobaki na kutokufanya makosa ambayo yanaonekana kuwagharimu wapinzani Wao.

Facebook Comments

Related posts