Chelsea walichezea “shilingi chooni”.

Nyota wa klabu ya Paris Saint Germain Kylan Mbappe alishawahi kufanya majaribio katika viunga vya Cobham mwaka 2012 lakini The Blues wakashindwana na mama yake baada ya kutaka afanyiwe tena majaribio.

Kwa sasa bwana mdogo Kylan Mbappe kashonyesha uwezo mkubwa akifanikiwa kuchuka Ligue 1 mara mbili pamoja na vikombe vingine vya nyumbani pale Ufaransa, Lakini alikuwa pia sehemu ya mafanikio ya Ufaransa kubeba kombe la dunia nchini Urusi. 

Mbappe akiwa na Pogba

Uwezo wake mkubwa uwanjani unamfanya kuwa mchezaji mwenye thamani ya juu PSG wakimchukua kwa njia ya mkopo Baadae inawagharimu €180 milioni ili kuwa mchezaji wao moja kwa moja.

Mpaka sasa mengi yameandikwa kuhusu Mbappe kuwa na upendo na Madrid lakini Chelsea ndo wa Kwanza kupata nafasi ya kumchukua Nyota huyo mchezaji bora mdogo kwenye kombe la dunia.

Mwaka 2012 mtafuta vipaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Serge Daniel Boga alimleta nyota huyo kwenye viunga vya Cobham na akaonyesha uwezo ila klabu ilishindwana mama yake baada ya kumuhitaji kufanya majaribio tena.

Boga aliuwambia mtandao wa Goal “Chelsea ndio klabu ya kwanza Kumpa Mbappe nafasi ya kufanya majaribio kabla ya Madrid, nilikuwa na rafiki anafanya kazi NIKE anaitwa Dennis Chantron na nlipokuwa Ufaransa tulikutana ushmsikia kijana mdogo anaitwa Mbappe? Anacheza klabu ndogo ya Bondy.

“Nikamwambia sijamsikia akaniambia unapaswa kumuangalia nikaenda kumwangalia, baadae nikamwambia rafiki yangu huyu kijana ana kitu.

“Baadae nikawaambia Chelsea kuhusu kijana na nikaita kila nliyekuwa nafanya naye kipindi hicho akiwemo Jim Fraser na kuwaambia sikiliza nnakijana huyu hapa mnapaswa kumuangalia.

“Nikamleta pale na familia yake na alionyesha uwezo kama alionao sasa, na alicheza dhidi ya Charlton na kushinda 7-0.

“Baada ya wiki Chelsea tukakutana Ofisini na kumwambia sikia tumefurahishwa na kiwango chako lakini tunakukaribisha tena kwaajili ya majaribio mengine na tutajua baada ya hapo.

“Nakumbuka mama yake alichosema siku ile, alizungumza Kifaransa na Fraser na nikawa na tafsiri, alisema mwanangu hawezi kurudia tena majaribio wakitaka watoe €50 million wamchukue sasa hivi kwa mkataba wa miaka mitano.

“Alijua thamani na uwezo wakijana wake ilitakiwa tu €50m. Na sasa unatoa €180m kwa hiyo alikuwa Sawa.

“Mpaka naamini Mbappe ni mchezaji bora kwangu kuwahi kumtafuta na nikimwangalia Najikuta nasema Wow macho yangu yalikuwa sawa kipindi kile.

Hata hivyo nafasi ya Chelsea kumsajili Mbappe Ndio ishapita kitambo hivyo.

Facebook Comments

Related posts