Swala la Rashford Kusugua benchi United liko hivi hayo mengine mnasema nyie.

Baada ya mechi za kimataifa vyombo vya habari nchini Uingereza vilikuwa vinadai kwamba Marcus Rashford hapati dakika nyingi za kucheza ndani ya kikosi cha Man United chini ya Mourinho na anatakiwa kuangalia mustakabali wake ili aendelee kucheza vizuri ndani ya kikosi cha England kama alivyofanya dhidi ya Hispania na Uswisi.

Leo kwenye mahojiano na vyombo vya habari , Mourinho inaonekana alijiandaa kuhusu hilo swali na amewapa jibu hili :

” Akiwa na mimi kama kocha wake katika misimu miwili , amecheza mechi 105 , dakika 5,744 , wastani wa mechi 63.7 kwa dakika 90 , pamoja na Fainali 5 ( Carabao, Ngao ya Jamii, FA Cup, Europa Ligi na UEFA Super Cup ) . Idadi kubwa ya mechi katika daraja la juu.”

” Kwahiyo watu wanaongea kuhusu dakika zake uwanjani chini yangu mimi nahisi wamechanganyikiwa. Yeye sio Solanke, yeye sio Loftus -Cheek na sio Calvert-Lewin.”

Facebook Comments

Related posts