Washindi Tuzo za FIFA 2018.

Tuzo za FIFA 2018 Zimetolewa katika hafla iliyofanyika katika Jiji la London Uingereza na Washindi wa Tuzo hizo ni hawa hapa. Luka Modric amechukua tuzo ya mchezaji bora FIFA 2018 akiwapiku Ronaldo na Mo Salah. Marta mwanamke wa Kibrazili amechukua Tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka. Kocha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa Didier Deschamp amechukua Tuzo ya Kocha Bora. Goli la Mosalah dhidi ya Everton limekuwa Goli Bora la mwaka huku mashabiki bora wa mwaka Tuzo ikienda kwa Mashabiki wa Peru.

Read More

FIFA awards La Liga kama wote.

Ligi kuu ya Spain (La Liga) imeendelea kutoa nyota wengi waliotwaa tuzo mbalimbali Katika tuzo za FIFA za mwaka 2018 kwa kutoa jumla ya wachezaji watano.  Kiungo Luka Modric ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2018 na kufanikiwa kuingia katika kikosi bora cha FIFA cha wachezaji 11.  Lakini pia mabeki wa tatu wa Real Madrid Raphael Varane, Sergio Ramos pamoja na Marcelo wameingia katika kikosi bora cha FIFA bila kumsahau mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na pengine unaweza kumjumuisha Cristiano Ronaldo anayekipiga Juventus kwa sasa ambaye amefanikiwa kuingia Katika…

Read More

Mshabiki Achezea Kichapo Baada ya kukimbia na Taulo la Kipa CCM Kirumba.

Michuano ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara imeendelea siku ya Leo kwa michezo mitatu kupigwa katika Viwanja vitatu tofauti. Moja Kati ya mechi Kali ni iliyopigwa katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza Mbao ikishinda goli 1-0 dhidi ya Wajelajela Tanzania Prison. Moja Kati ya tukio lilitokea katika mchezo huo ni katika DK ya 80 mshabiki mmoja kuchukua taulo la Kipa wa Prison na kukimbia nalo na Maafande wa jeshi la Magereza kumkamata na kumpa kichapo kabla ya askari Polisi waliokuwa uwanjani kuja kumchukua na kumpakia kwenye gari lao. Baadhi ya…

Read More

Mwanafunzi wa Sekondari anaswa kwa tuhuma za kutupa kichanga chooni.

MWANAFUNZI AJIFUNGUA NA KUTUPA MTOTO CHOONI Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Isengo, Ines Mtundu (19) anamshikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kosa la kumtupa chooni mtoto mchanga baada ya kujifungua. Picha ya Mtoto Taarifa ya tukio hilo imetolewa leo tarehe 24 Septemba 2018 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Mate wakati akizungumza na wanahabari. “Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 23.09.2018 majira ya saa 09:53 asubuhi huko maeneo ya Isengo – Airport ya zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini…

Read More

Nape anusurika Kifo.

  Mbunge wa Mtama kupitia CCM Nape Moses Nauye, amenusurika kifo baada ya gari Aina ya Land Cruiser Vx yenye namba 349 DEL alilokuwa amepanda kupinduka majira ya saa Moja na nusu asubuhi ya Leo hii katika Kijiji cha Kibutuka kilichopo wilayani Liwale Mkoani Lindi. Nape alikuwa anaelekea Liwale katika ziara ya Katibu mkuu wa Ccm Dr Bashiru Ally. Katika ajali hiyo hakuna aliyeumia isipokuwa gari lake ndio limeharibika sana eneo la mbele.  

Read More

Woods amerudi.

Bingwa wa zamani wa Dunia wa mchezo wa Golf Tiger Woods amefanikiwa kushinda Michuano ya Tour Championship likiwa ni taji lake la kwanza ndani ya miaka mitano. Woods Ana umri wa miaka 42 hivi sasa na taji hili alilolitwaa pale Atlanta linamfanya arudi mchezoni baada ya kuwa amekamata nafasi ya 1,199 katika viwango vya ubora ikiwa si chini ya mwaka mmoja tangu afanyanyiwe upasuaji wa matatizo ya Uti wa mmgongo. Mkongwe Tiger Woods bingwa wa mataji 14 makubwa ya Golf mara ya mwisho kushinda mashindano ilikuwa August 2013 katika mashindano…

Read More