Woods amerudi.

Bingwa wa zamani wa Dunia wa mchezo wa Golf Tiger Woods amefanikiwa kushinda Michuano ya Tour Championship likiwa ni taji lake la kwanza ndani ya miaka mitano.

Woods Ana umri wa miaka 42 hivi sasa na taji hili alilolitwaa pale Atlanta linamfanya arudi mchezoni baada ya kuwa amekamata nafasi ya 1,199 katika viwango vya ubora ikiwa si chini ya mwaka mmoja tangu afanyanyiwe upasuaji wa matatizo ya Uti wa mmgongo.

Mkongwe Tiger Woods bingwa wa mataji 14 makubwa ya Golf mara ya mwisho kushinda mashindano ilikuwa August 2013 katika mashindano ya WGC-Bridgestone Invitational.

Related posts