Ugunduzi: Mwanafunzi wa Namibia agundua simu isiyotumia vocha wala laini

Simon Petrus Mwanafunzi wa Sekondari nchini Namibia, amegundua simu isiyotumia vocha wala kadi, kijana huyo  ameuelezea ugunduzi wake kuwa unatumia mawimbi ya redio na hauhitaji kuwa na ‘simcard na airtime’.

Simon amesema ugunduzi huo  umetumia miaka 2 kukamilika ambapo ametumia  mabaki ya simu na runinga zilizoharibika.

Wazazi wake ambao hawana ajira kwa sasa walihangaika kumsaidia kijana wao ili akamilishe mradi huo uliogharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni Nne.

Simon petrus aliyekaa katikati

Related posts