Hazard aweka ngumu Klopp nje Carabao Cup.

Emerson na Hazard wamepeleka kilio kwa vijana wa Jurgen Klopp ndani ya Anfield mechi ya kombe la Carabao. Danny Sturridge kafunga goli la kufutia machozi : Chelsea wanasonga mbele , Liverpool wanabaki nyumbani. Endapo Klopp angepata ushindi ungekuwa ushindi wake wa nane mfululizo lakini uwezo binafsi wa Hazard aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Willian ukaisaidia The Blues kupata ushindi wa goli 2-1 ugenini.  

Read More

WILLY PAUL na BAHATI Wanatuhumiwa kutokuwalipa “Video Vixens”

TATIZO hili la kukwepa kutimiza haki za Warembo wanaotumika katika Video za wasanii mbali mbali (Video Vixens/Video Queens) katika malipo yao, zilikuwa zikiwaandama wasanii kadha wa kadha wa Tanzania kwa asilimia kubwa, lakini kumbe hata nchini Kenya, kuna majina makubwa ya wasanii ambao huwanyima pesa zao warembo hao Msanii wa Gospel Nchini Kenya WILLY PAUL na mwenzake BAHATI , wameingia katika kashfa ya kutokuwalipa Video Vixens ambao wanafanya nao kazi, licha ya kwamba video zao huwa zinafanikiwa na wao kuvuna pesa nyingi sana Mmoja kati ya Warembo hao, ambaye uvumilivu…

Read More

HAMISA MOBETO : “Nilimuonea Huruma Diamond,Sikuwa na Uwezo wa Kumsaidia”

“MADAM HERO” Hamisa Mobeto bado yuko Nchini Kenya na Siku ya Kesho atakuwa na shughuli ya “mkwanja” huko huko akionesha kupambana kama ambavyo alituambia kupitia Track yake ya “Madam Hero” Kama ambavyo unafahamu, Hamisa ameshaamua kufunguka kila anapoulizwa kuhusu Maisha yake na Diamond Platnumz ambaye ni mzazi mwenzake kwa hivi sasa, Ugomvi wao, Masuala ya Ushirikina na kadhalika, tofauti na siku chache hapo nyuma baada ya ishu za kumroga hitmaker huyo wa “iyena” zianze kuzagaa.   Akiwa Nchini Kenya, Hamisa ameweka wazi kama pengine kuna kitu ambacho kilimvutia kwa Diamond…

Read More

#KENYA : GAVANA “Kikaangoni” kwa Kunywa Chai huku Wanafunzi Wakimtizama

UKITIZAMA tu hii picha, mwenyewe utajiuliza Swali hili “Hivi Kweli Gavana huyu alikuwa anafurahia Kifungua Kinywa Huku Wanafunzi wanamtizama?” na kiuhalisia hii ndiyo hali ambayo imemfanya ajikute katika kikaango Kizito. Gavana wa  Eneo la Pokot Magharibi , JOHN LONYANGAPUO ( Wa Tatu Kutoka Kulia , aliyevalia Koti la Blue Bahari) amejikuta akishambuliwa na raia wengi wa Nchi ya Kenya, baada ya kuonekana akifurahia “kifungua Kinywa” huku wanafunzi wakimtizama kuashiria kuwa wana hamu na chai Hiyo ama wanahisi Njaa Tukio hilo ambalo limetokea katika Shule ya Msingi Kitalaposho iliyoko katika Kata…

Read More

GOOGLE CHROME INAFANYA UDUKUZI KATIKA ACCOUNT ZA WATU?

KAMA utakuwa ni mtumiaji wa account ya gmail ambayo iko chini ya Kampuni ya Google, basi utakuwa umefahamu ama kubaini kuwa kuna mabadiliko katika “Google Chrome”, sehemu ambayo huwa tunaitumia kutafuta taarifa mbali mbali (search Engine). Mabadiliko hayo mapya ambayo yameboreshwa hivi Karibuni, kama utakuwa  umeingia katika email account yako kisha ukafungua “google Chrome” basi utaona kwa pembeni kuwa uko Online moja kwa moja na huenda taarifa zako zinatumwa moja kwa moja katika email yako bila wewe kuidhinisha ama kuruhusu kitu hicho Profesa Green kutoka Taasisi ya JOHNS HOPKINS INFORMATION…

Read More

Kabila asisitiza chaguzi za amani Congo zitafanyika Desemba 23

  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jospeh Kabila amesisitiza kuwa uchaguzi nchini mwake utafanyika tarehe 23 Desemba na kwamba hilo haliwezi kubadilika. Kabila ameshutumu vikali muingilio wowote katika mchakato huo wa uchaguzi kutoka mataifa ya kigeni. Akizungumza jana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Rais Kabila amesema kila kitu kitatekelezwa kuhakisha chaguzi zinaendeshwa kwa amani, na kwa njia za haki. Kabila ameonya kuwa Umoja wa Mataifa hakitakuwa chombo kinachowajumuisha wote iwapo mataifa ya kigeni yataendeleza uingiliaji kati kwenye masuala ya ndani ya nchi…

Read More

Macron aushutumu mtizamo wa Trump wa ‘mwenye nguvu mpishe’

  Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amewaomba viongozi wa dunia kupinga kile alichokitaja sheria ya mwenye nguvu kuliko wote, akikosoa vikali mtizamo wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kushughulikia kivyake changamoto zinazoukumba ulimwengu. Macron hakumtaja kwa jina Trump, lakini hotuba yake hapo jana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alianisha misimamo ambayo ni tofauti kabisa na mtizamo alionao rais huyo wa Marekani. Macron amesema baadhi ya viongozi wameamua kufuata sheria ya mwenye nguvu mpishe, lakini hilo haliwezi kumlinda yeyote, badala yake anaunga mkono ushirikiano na mashauriano yanayoshirikisha pande…

Read More

MCHEKESHAJI BILL COSBY KWENDA GEREZANI KWA UBAKAJI

Bill Cosby Mcheshi nguli Bill Cosby raia wa Marekani huenda akakaa gerezani kwa muda wa miaka 3 – 10 kwa ubakaji . Cosby ameshtakiwa kwa dhuluma za kimapenzi dhidi ya bi Andrea Constand mfanyikazi wa chuo kikuu kimoja nchini Marekani. Kosa hilo yamkini lilifanyika mwaka wa 2004. Bi Andrea aliishawishi mahakama kuwa Cosby alimpa dawa aina ya Quaaludes ambayo ilimlegeza na hakuweza kumzuia kumbaka mwaka wa 2004.

Read More