Kiasi anachotoa Mpakistani kuinunua Wembley Kesho.

Hatimaye chama cha soka nchini Uingereza kimeupiga bei uwanja wao Taifa Wembley kwa klabu ya Fulham na mmililki wa Jacksonville Jaguars Shahid Khan kwa dau la £600 milioni na hiyo ni kwa mujibu wa jarida la Financial Times.

Tangu Mwezi April Mfanyabiashara huyo wa Kipakistan amekuwa kwenye mazungumzo ya kuununua uwanja huo na hatimaye deal hilo kubwa limekubaliwa.

Kwa sasa tunasubiri Alhamisi ambapo wawakilishi 10 kutoka FA watakutana kwenye kikao cha Bodi kupitisha Ombi hilo.

Kama kikao hicho cha Bodi kitakubaliana na ombi la Khan basi biashara hiyo itawasilishwa kwenye kikao cha FA chenye wawakilishi 127 ili kukubaliana kwenye kikao cha Mwezi unaofuata.

 

Related posts