Kipigo cha aina hii ni Mara ya kwanza tangu 2015 La Liga.

Kwa mara ya kwanza tangu January 2015 Vigogo wa Soka Nchini Spain Barcelona na Real Madrid wanafungwa wote katika siku moja kwa vichapo toka kwa Sevilla na Leganes siku ya Jumatano.

Mabingwa na vinara wa LA Liga wakajikuta wanachapwa 2-1 pale Butarque kwa Goli la mchezaji wa mkopo toka Madrid Oscar Rodriguez aliyeifungia Leganes goli la ushindi Baada ya makosa ya Beki Gerard Pique.

Madrid nao wakawa na nafasi ya kukwea kileleni lakini kichapo makini cha goli 3-0 toka kwa Sevilla kikakwamisha ndoto za Kocha Julen Lopetegue.

Baada ya mzunguko wa sita sasa vilabu hivyo Vigogo vyote viko sawa kwa alama 13 huku vijana Ernest Valverde wakiwa juu kwa utofauti wa magoli.

 

Related posts