Maalim Seif Sharrif Hamad kugombea Kiti cha urais 2020

Baraza la Wazee la Chama cha Chadema limebainisha mipango ya kumshawishi Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) na Makamu wa kwanza wa zamani wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (2010-2015), Maalim Seif Sharrif Hamad kuwa mgombea wao katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 visiwani Zanzibar. Tamko la Wazee wa Chadema lililotolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashimu Issa Juma, limekuja katika kipindi ambacho chama cha CUF kimekumbwa na mgogoro wa uongozi tangu mwaka 2015. Hii ni baada ya aliyekuwa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu wadhifa wake kuelekea uchaguzi…

Read More

Sababu za Man kuchezea kichapo hizi hapa.

Jumamosi hii kwenye Ligi kuu ya soka Uingereza mambo sio mazuri kwa Mashetani wekundu Manchester United baada ya kuchezea kichapo cha Goli 3-1 toka kwa Westham United (Wagonga nyundo kutoka Londoni). Huu ni Mchezo wa pili mfululizo Man U wanapoteza ndani ya wiki moja wakitoka pia kufungwa na Derby County kwenye Carabao Cup ila pia ni Mchezo wa tatu wanafungwa Katika Ligi kuu msimu huu. Kocha wa Manchester United amewarushia lawama waamuzi wa Mchezo huo akisema hawakuyaona makosa Katika magoli mawili waliyofungwa. Kuhusu timu kutokucheza Vizuri amesema nikutokana na baadhi…

Read More

JEMBE FM YASISITIZA UKARIBU WA WAZAZI KWA WANAFUNZI

“Sisi kama Jembe Fm tunatambua kuwa mnafundishwa mengi na walimu wenu ili kuhakikisha mnafaulu masomo, hata hivyo tunaongeza kwa kusema Elimu ni jambo moja lakini unaitumiaje Elimu ni jambo jingine, ndio maana tunasisitiza kuendelea kuwa karibu na wanafunzi na kuwaelekeza ni njia gani wapite ili kutimiza malengo hasa kwa kujiajiri ” Harith Jaha, mkuu msaidizi wa vipindi @jembefm Mwanza alipokuwa akiongea na wanafunzi wa shule za kidato cha tano na sita zilizopo jijini Mwanza katika viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana ya Loreto iliyopo jijini Mwanza katika hafla iliyoandaliwa…

Read More

Watu zaidi ya mia tatu wapoteza maisha ,ni baada ya kuibuka kwa tsunami.

Takribani watu 384 wamethibitishwa kufariki baada ya tsunami kubwa iliyosababishwa na tetemeko la aridhi kuikumba pwani ya Indonesia, Mashuhuda katika eneo la Sulawesi wanasema mawimbi yenye kimo cha mita tatu hivi yalikumba maeneo yaliyo karibu na ufukwe wa bahari na kusababisha uharibifu mkubwa wa miondo mbinu Jeshi la taifa hilo limeanza mikakati ya uokoaji huku idadi ya waliofariki ikitarajiwa kuongezeka.

Read More

RWANDA NA ISRAEL ZAFUNGUA UKURASA MPYA WA KIDIPLOMASIA

Serikali ya Israeli 🇮🇱 imekubaliana na Rwanda 🇷🇼 kufungua ubalozi wake jijini Kigali hivi karibuni katika jitihada za kuimarisha mahusiano baina yao. Kauli hii ilifikiwa katika mkutano wa faragha kati ya rais wa Rwanda Paul Kagame na waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kandokando ya mkutano mkuu wa mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa UN huko New York Marekani. #rwanda #israel 📸:Paul Kagame. #Chanzobbcswahili

Read More

Waziri wa mambo ya Nchi za Kigeni wa Ujerumani Heiko Maas amelitaka Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hatimaye kuanzisha mazungumzo muhimu kuhusu mageuzi katika Baraza la Usalama la umoja huo

  Maas amesema Baraza hilo halijabdilika tangu lilipoasisiwa mwaka wa 1945, licha ya kuongezeka mara tatu kwa idadi ya watu duniani tangu wakati huo, na kuongezeka mara nne idadi ya nchi wanachama katika kipindi hicho. Ujerumani kwa muda mrefu imekuwa ikishinikiza megeuzi ya Umoja wa Mataifa na lengo kuu la kutaka kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama. China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani ni wanachama wa kudumu wakiwa na kura za turufu kuhusu maamuzi ya Baraza hilo. Ujerumani imechaguliwa kuwa mmoja wa wanachama 10 wasio wa kudumu kwa muhula…

Read More

FAST JET SASA KUJIENDESHA, NI BAADA YA KUSITISHIWA UFADHILI

Dar es Salaam. Kampuni ya ndege ya Fastjet Plc ya Uingereza inapanga kusitisha ufadhili wake kwa Fastjet Tanzania. Hali hiyo inatokana na mwenendo mbaya wa biashara uliosababisha ukata katika kampuni hiyo, lakini Fastjet Tanzania imewatoa wasiwasi wateja wake na kueleza kuwa itaendelea kutoa huduma kama kawaida. Juzi, Fastjet Plc ilitoa taarifa ya mwenendo wake wa fedha kuwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha kiasi cha kulazimika kuzitafuta kwa kufanya harambee na endapo hazitatosha basi itasitisha huduma zake nchini. “Tunazungumza na wanahisa kufanya harambee kupata fedha ya ziada. Kwa hali ilivyo,…

Read More

HALI SI SHWARI NI KWA WAKIMBIZI WA VISIWA VYA UGIRIKI BAADHI WAHOFIWA KUJIUA

Maelfu ya wahamiaji walio kwenye makambi yaliyojaa katika visiwa vya Ugiriki wanasubiri kwa wasiwasi majira ya baridi hali ambayo tayari imewafanya baadhi ya watu hao kujaribu kujiua. Hata wale waliomo kwenye orodha ya kuhamishwa kupelekwa bara baada ya mashirika yasiyo ya kiserikali kufichua hali duni katika kambi hizo wanaomba na kujenga matumaini kwamba safari yao iwe kabla ya mvua za msimu hazijaanza na kuigeuza kambi yao kuwa dimbwi la matope. Mkimbizi mmoja mwenye umri wa miaka 53 Jamal ambaye anaishi kwenye kambi ya Moria katika kisiwa cha Lesbos anauliza kwa…

Read More