JEMBE FM YASISITIZA UKARIBU WA WAZAZI KWA WANAFUNZI

“Sisi kama Jembe Fm tunatambua kuwa mnafundishwa mengi na walimu wenu ili kuhakikisha mnafaulu masomo, hata hivyo tunaongeza kwa kusema Elimu ni jambo moja lakini unaitumiaje Elimu ni jambo jingine, ndio maana tunasisitiza kuendelea kuwa karibu na wanafunzi na kuwaelekeza ni njia gani wapite ili kutimiza malengo hasa kwa kujiajiri ”

Harith Jaha, mkuu msaidizi wa vipindi @jembefm Mwanza alipokuwa akiongea na wanafunzi wa shule za kidato cha tano na sita zilizopo jijini Mwanza katika viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana ya Loreto iliyopo jijini Mwanza katika hafla iliyoandaliwa kwa lengo la kuwajenga wanafunzi kisaikolojia ili kutimiza ndoto zao.

Related posts