Maalim Seif Sharrif Hamad kugombea Kiti cha urais 2020

Baraza la Wazee la Chama cha Chadema limebainisha mipango ya kumshawishi Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF)

na Makamu wa kwanza wa zamani wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (2010-2015), Maalim Seif Sharrif Hamad kuwa mgombea wao katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 visiwani Zanzibar.

Tamko la Wazee wa Chadema lililotolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Hashimu Issa Juma, limekuja katika kipindi ambacho chama cha CUF kimekumbwa na mgogoro wa uongozi tangu mwaka 2015.

Hii ni baada ya aliyekuwa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu wadhifa wake kuelekea uchaguzi mkuu kisha mwaka 2017 kurejea kwenye cheo hicho kinyemela licha ya kueleza kuwa baadhi ya wanachama wamemuomba arudi madarakani.

Kurudi kwa Lipumba ndani ya Cuf kumetengeneza makundi mawili. Kundi la wanaomuunga mkono Profesa huyo na jingine likiwa upande wa Maalim Seif


 

Related posts