Sababu za Man kuchezea kichapo hizi hapa.

Jumamosi hii kwenye Ligi kuu ya soka Uingereza mambo sio mazuri kwa Mashetani wekundu Manchester United baada ya kuchezea kichapo cha Goli 3-1 toka kwa Westham United (Wagonga nyundo kutoka Londoni).

Huu ni Mchezo wa pili mfululizo Man U wanapoteza ndani ya wiki moja wakitoka pia kufungwa na Derby County kwenye Carabao Cup ila pia ni Mchezo wa tatu wanafungwa Katika Ligi kuu msimu huu.

Kocha wa Manchester United amewarushia lawama waamuzi wa Mchezo huo akisema hawakuyaona makosa Katika magoli mawili waliyofungwa.

Kuhusu timu kutokucheza Vizuri amesema nikutokana na baadhi ya wachezaji wake kutokuonyesha hari ya kujituma na kucheza.

Related posts