Wana Jangwani mnakumbuka April 29 mwaka huu?

Leo ndio leo uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam wanasema “mtoto hatumwi dukani” kwanzia saa 10 jioni muda rafiki kwa watanzania kushudia mechi, itaanza mechi Kali ya watani wa jadi Simba dhidi ya Yanga.

Kuelekea mchezo huu tukumbushane kwamba timu hizi kabla ya Mchezo wa leo kihistoria zimekutana mara 103, Yanga ikishinda mara 38 na Simba mara 33 nakutoka sare mara 32, katika hiyo michezo yote klabu ya Yanga imefunga magoli 105 wakati Simba imefunga magoli 95.

Mara ya mwisho kukutana timu hizi mbili ni April 29 ambapo yanga ilichezea kichapo cha Goli 1-0 na goli likifungwa na mkongwe Erasto Nyoni.

“Ngoma ya vijana haikeshi” Leo yanga wanalipiza kisasi au?

Related posts