Kiwango cha Barkley chamkuna Carragher.

Nyota wa Klabu ya Chelsea anayekuja juu hivi Sasa Ross Barkley anaweza kuwa muhimili mkubwa Katika kikosi cha Timu ya taifa ya England chini ya kocha Gareth Southgate kwa mujibu wa mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher. Kiungo huyo wa Chelsea alifanikiwa kucheka na nyavu wikendi iliyopita ikiwa ni katika michezo mitatu mfululizo kufanya hivyo na Carragher anaamini nyota huyo wa zamani wa Everton ataonyesha ubora huo pia Katika taifa. Ukifananisha uwezo wa sasa wa Barkley na alivyokuwa Everton, Carragher anadai uwezo wamchezaji huyo umekuwa zaidi kwa sasa.

Read More

Besiktas hichi ndicho wanachotaka kumfanyia Karius.

Zimetoka taarifa kuwa Klabu ya Besiktas ya Uturuki ipo mbioni kuukatisha mkataba wa mkopo wa Loris Karius ili mlinda mlango huyo arejee kwenye Klabu yake ya Liverpool.   Kwa Mara ya kwanza Karius amekaa langoni kuidakia Besiktas ni Katika mechi dhidi ya Bursaspor iliyomalizika kwa sare ya 1-1 mchezo ulipigwa Sept 2. Tangu hapo Karius amekaa kwa ujumla mara 11 akiruhusu nyavu zake kuguswa mara 16, akiwa ameisaidia timu yake kushinda michezo mitano akiwa langoni na wakitoka sare 3 na timu kufngwa mara yeye akiwa langoni. Mkataba wa mkopo wa…

Read More

Kuelekea mchezo na Lipuli leo Taifa Yanga anabebwa na rekodi hizi mbili.

Yanga Katika michezo yao yote waliyohesabika kuwa wapo nyumbani msimu huu imeisha kwa wao kugawa dozi ya vipigo. Leo wapo Taifa dhidi ya Lipuli ambayo imetoka kanda ya ziwa wakibeba alama tatu Baada ya kuifunga Klabu ngumu ya Mbao Msimu huu Katika mchezo wao wa mwisho uliopigwa CCM kirumba. Mchezo unapigwa kwanzia saa 1 usiku na Yanga watajaribu kuendeleza record yao yakushinda nyumbani msimu huu na record ya kutokupoteza mchezo wowote Msimu huu Katika ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Read More

Baada ya kusambaza vipigo hatimaye Raptors akutana na kisiki.

Baada ya kuanza Msimu huu wa mpira wa kikapu nchini Marekani NBA vizuri kwa kugawa dozi kwa kila timu iliyokuwa inawasogelea Hatimaye Raptors wamepatikana baada ya kucharazwa kwa alama 109-124 dhidi ya Bucks. Kabla ya mchezo huu alifajiri ya leo Raptors walikuwa wamecheza mechi sita za awali bila kupoteza lakini pia ni ushindi wa saba mfululizo kwa klabu ya Bucks. Matokeo mengine ya NBA Leo 

Read More

Lopetegui rasmi atimuliwa Madrid baada ya kuingoza kwenye mechi 14 tu.

Hatimaye Klabu ya Real Madrid imemfungashia virago aliyekuwa kocha wake Julen Lopotegui baada ya kuingoza Madrid kwa takribani mechi 14, na hili limejiri Baada ya kupokea kisago cha goli 5-1 toka kwa Barca wikendi iliyopita. Santiago Solar ambaye alikuwa akipendekezwa kurithi mikoba ya Lopotegui kwa muda, sasa amepewa nafasi hiyo. Real Madrid wameshindwa kupata ushindi kwenye LA Liga tangu wamfunge Espanyol September 22 baada ya hapo wakapoteza dhidi ya Sevilla,  Alaves, Levante na kutoka sare na Atletico Madrid kabla ya Kipigo kizito cha goli 5-1 toka kwa Barca. Lopotegui mwenye…

Read More

WANAOSAMBAZA VIDEO NA PICHA ZA NGONO KUKIONA

  Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imeapa kula sahani moja na wale wote wanaosambaza video au picha za ngono katika mitandao ya kijamii. Mamlaka hiyo imesisitiza kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kutenda makosa hayo. Hatua hii inakuja ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ya msanii Wema Sepetu pamoja na ya binti mwingine maarufu kwa jina la Amber rutty zenye maudhui ya ngono.

Read More

GAZETI LA TANZANITE KITANZINI, NI BAADA YA KUANDIKA HABARI ZILIZOZUA UTATA

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema habari iliyochapishwa na gazeti la kila siku la Tanzanite la leo Jumatatu tarehe 29 Oktoba, 2018 lenye habari zenye tuhuma za kisiasa dhidi ya Viongozi kadhaa, haziakisi msimamo wa Serikali na ameagiza mmiliki na Bodi ya uhariri ya gazeti hilo waitwe mara moja Idara ya Habari (MAELEZO) kujieleza kuhusu msingi wa habari hiyo. Dkt. Mwakyembe ametoa ufafanuzi huo leo mchana, mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuelezea kushtushwa kwake na…

Read More

Ajali ya Helicopter Mbali na kumchukua mmiliki wa Leicester City imeondoka na Mrembo.

Baada ya kuthibitishwa kifo cha bilionea wa Kithailand na mmiliki wa Klabu ya Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha ambae alifariki kutokana na ajali ya Helicopter iliyotekea Jumamosi nje ya uwanja wa King Power Stadium waliofariki wengine wametambulika. Mmoja Wapo wa waliofariki ni Mrembo Nusara Sukinamai ambaye alishawahi kushiriki mashindano ya Miss Thailand Universe. Baadhi ya wadau wametoa salamu zao za rambirambi kuhusu kifo Cha Vichai ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Leicester City. “Ulikuwa mtu wa kufariji Kila mtu pasipo wezekana kuwezekana” Maneno ya kipa wa Leicester City,  Schmeichel.

Read More