Mourinho “kuna wachezaji hawajali hali ya timu”.

Kwa sasa hali si shwari pale Old Trafford ambapo Kocha Jose Mourinho amekuwa akiwatupia maneno wachezaji wake ambapo ameweka wazi kwamba kuna wachezaji wanasumbuka kuisaidia klabu Katika kipindi hiki kigumu na kuna ambao hawafanyi hivyo.

Manchester United mpaka sasa wapo nafasi ya 10 ya msimamo Katika Ligi kuu na Matokeo ya kufungwa 3-1 na Westham Wikendi ilyopita yakizidi kumuumiza Kocha huyo wa Kireno.

Baada ya kufanya vibaya na kuambulia kichapo hicho kuna wachezaji wanaonekana chanzo cha Tatizo na hasa anatajwa Paul Pogba amabaye maelewano yake na Mourhno sio mazuri.

Na Mourhno bila kutaja majina mengine ya wachezaji anasema tu kuna wachezaji hawajali kinachoendelea Katika timu na kuna ambao wanajali.

“Naona watu walio tofauti, kuna ambao hawaonekani kubabaishwa na timu kupoteza” Alisema Mournho.

Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid pia anaamini ni jukumu la Kila mmoja Katika timu kupambana kubadilisha hali ilivyo hivi Sasa.

Morinho anamchezo Leo wa Ligi ya mabigwa dhidi ya Valencia na amethibitisha kuwa Kosa wachezaji baadhi kulekea Mchezo huo, wachezaji hao ni Marcos Rojo, Ander Herrera, Jesse Lingard na Ashley Young. 

Facebook Comments

Related posts