HATMA YA DHAMANA YA MGOMBEA URAISI RWANDA SASA MIKONONI MWA MAHAKAMA

Mahakama mjini Kigali leo inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kuachiliwa huru kwa dhamana kwa mwanasiasa Diane Rwigara aliyekuwa ametangaza nia ya kuwania urais dhidi ya rais Paul Kagame katika uchaguzi uliopita.
Diane na mamake Adeline Rwigara wanakabiliwa na makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka. Wote wamekanusha madai hayo wakisema yalichochewa kisiasa.

Facebook Comments

Related posts