Hamilton alinyatia taji la tano sasa Formula One.

Dereva wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton yu mbioni kutawazwa kuwa bingwa wa Dunia kwa mara ya tano Katika michuano ya mbio za magari Formula 1 baada ya kuibuka mshindi kwenye michuano ya Japan GP.

Matokeo hayo mazuri kwa Hamilton yanamaanisha Dereva wa Ferrari Sebastian Vettel Sasa ameachwa kwa alama 67 na muingereza huyo.

Sasa muingereza Hamilton atatawazwa kuwa bingwa rasmi atakaposhinda mashindano ya US GP wiki mbili zijazo endapo ataibuka wa kwanza au wa pili.

 

Facebook Comments

Related posts