Baada ya miaka 23 Terry avunja ndoa soka.

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya England na klabu ya Chelsea, John Terry ametangaza rasmi kustaafu soka na hatua hiyo inakuza mjadala wa yeye kuunganza na Thierry Henry kwenye bechi la ufundi la Aston Villa.

Baada ya kulitumikia soka kwa muda mrefu kama Mchezaji kwa takribani miaka 23 akicheza mechi takribani 800 Terry anaona ni muda muafaka kutundika daluga.

Tutamkumbuka zaidi kwa miaka 19 aliyoitumika Chelsea kama beki kisiki akiiwasaidia wana darajani kutwaa mataji 17 ukijumuisha mataji matano ya Premier League.

Baada ya kuondoka Chelsea FC akaitumika Aston Villa kwa mwaka mmoja akiwa nahodha na baada ya hapo akahusishwa kwenda Spartak Moscow na hakwenda na sasa anatazamia maswala ya ukocha.

Huku Mchezaji wa zamani wa Ufaransa na klabu ya Arsenal, Thierry Henry akihusishwa kuchukua mikoba ya kocha Steve Bruce Katika klabu ya Aston Villa,  Terry inasemekana atakuwa Msaidizi wake.

Facebook Comments

Related posts