Ethiopia wasubiri kichapo toka kwa Harambee Stars Kesho kutwa.

Mataifa ya Ghana, Kenya na Ethiopia kwa pamoja yanaunda Kundi F Katika michuano ya kuwania fainali za Mataifa ya Africa baada ya Sierra Leone kufungiwa na FIFA baada ya serikali yao kuingilia maswala ya soka.

Mshambuliaji wa Harambee Stars Allan Wanga anaamini Kenya inakila sifa ya kuwacharaza Ethiopia siku ya Jumatano.

Taifa la Kenya lina mipango ya kukusanya point wanapo safiri kuumana na majirani zao hao ilikupata nafasi ya kukaa kileleni mwa Kundi F kwa idadi ya alama sita.

Na Mshambuliaji huyo wa Kakamega Homeboyz anaamini hayo ni malengo ya Taifa Kipindi hiki amabacho wanaangalia kufuzu AFCON kwa mara ya kwanza tangu 2004.

Facebook Comments

Related posts