Hazard “nikiondoka Chelsea ntafurahi”.

Nyota wa klabu ya Chelsea Eden Hazard amedai anajikuta kwenye Wakati mgumu kuamua kipi afanye ahamie Madrid au aongeze mkataba mpya darajani akiweka wazi kutumikia Madrid ni ndoto yake tangu utotoni.

Chelsea wanapambana kumuongezea Mbeligiji huyo mkataba mpya kabla kukumbwa navishawishi Mwezi January toka Madrid lakini Hazard mwenyewe bado hajakubaliana na hilo huku akiwa amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa.

Hazard ndie Mchezaji anaengoza kwa magoli kwenye Premier League kwa sasa akiwa na magoli saba baada ya kufunga kwenye Mchezo uliopita timu yake ikishinda 3-0 dhidi ya Southampton siku ya Jumapili.

“Ni kama nlivyokuwa nasema mara nyingi kwamba kama nikiondoka nitakuwa na furaha, najua hata nikibaki ntakuwa nafuraha. Sio kama nikiondoka ninafuraha kama nikibaki sina furaha” maneno ya Hazard hayo.

 

Facebook Comments

Related posts