Ligali aitema timu ya Taifa ya Ufaransa afuata Taifa la Mama yake.

Mlinda mlango wa zamani timu ya Taifa ya vijana ya Ufaransa chini umri wa miaka 20 kwenye michuano ya Kombe la Dunia, Jonathan Ligali amechukua maamuzi ya kuachana na timu hiyo na kulitumikia Taifa la Benin.

Ligali kachukua maamuzi hayo ikiwa ni kama kuonyesha heshima kwa mama yake ambaye ni raia wa Taifa hilo kutoka barani Afrika.

Kwa utaratibu wa FIFA yupo Sawa kuhama kwa Sababu ilikuwa bado hajatumikia timu ya Ufaransa ya wakubwa.

Kwenye Mahojiano Ligali anaesma “me nipo tayari kuitumikia Benin kama wakinihitaji”.

Ligali mwenye miaka 27 anaitumikia klabu ya Montpellier ya Ufaransa hajawahi kuitumikia timu ya wakubwa ya Ufaransa.

Facebook Comments

Related posts