MUANDISHI WA HABARI KORTINI KWA MAUAJI.

Mwandishi wa habari wa runinga ya Citizen ya Kenya Jackie Maribe na mchumba wake Joseph Irungu sasa watapandishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Wawili hao wamekuwa kizuizini toka mwezi uliopita kupisha polisi kufanya uchunguzi wa kifo cha mfanyabiashara Monica Kimani, aliyeuawa kwa kukatwa shingo Septemba 19 katika nyumba yake jijini Nairobi.

Baada ya uchunguzi wa wiki tatu, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Kenya Noordin Haji ameagiza wawili hao kufikisha Mahakama Kuu mara moja na kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Facebook Comments

Related posts