RITHA KAGGWA KWA EDDY KENZO : “Nilikupa Hifadhi Nyumbani Kwangu”

VITA ya kurushiana maneno baina ya Msanii kutoka nchini Uganda Eddy Kenzo na Blogger Ritha Kaggwa ambaye makazi yake ni Nchini Uingereza inazidi kuchukua nafasi yake katika mitandao ya kijamii, hali ambayo imeanza kupelekea mpaka kufichuliana siri ambazo hatukuwa tukizifahamu

PICHA LILIANZA HIVI….

Mnamo October 6, Blogger huyo Ritha Kaggwa, alipost taarifa kupitia “Facebook Fan Page” yake, ambayo ilikuwa ikimtuhumu Eddy Kenzo kumtelekeza mke wake Remma Namakulah (ambaye pia ni msanii) pamoja na mtoto wao, na kukimbilia Nchini Marekani ambako inasadikika kuwa alikuwa akiishi na mwanamke mwingine anayeitwa SALMA

Taarifa hiyo iliyoandikwa na Bi Kaggwa, alivujishiwa na “shushushu” ambaye aliomba afichiwe utambulisho wake na anaishi maeneo ya Boston ila alitumia jina moja tu la CYNTHIA

Pia mvujiashaji huyo akaongeza kuwa, Salma ambaye anatajwa kuwa ni Mpenzi wa Eddy Kenzo, ana ujauzito wa miezi mitatu na huo ujauzito ni wa Msanii huyo

Sasa, baada ya Eddy Kenzo kuipata taarifa hiyo, alihoji kwa waungwana kama kuna mtu yeyote anamfahamu Ritha Kaggwa, blogger ambaye ameandika taarifa hiyo, na kisha kumtishia kwa kumwambia kuwa atamkata midomo yake

Eddy Kenzo aliandika  Hivi

” Ni Nani anamfahamu mwanamke anayeitwa Ritha Kaggwa?. Nitamkata Midomo yake”

ALICHOKIJIBU RITHA KAGGWA

Blogger huyo ambaye hivi karibuni amefunga ndoa huko huko nchini Uingereza na akimalizia Fungate yake (Honeymoon) aliamua kumtolea uvivu Eddy Kenzo hasa baada ya kuona kuwa Mshindi huyo wa Tuzo ya AFRIMMA 2018 anakana kufahamiana naye

Eddy Kenzo (Kushoto) na Ritha Kaggwa wakiwa London

Bi Kaggwa aliweka wazi kuwa Eddy Kenzo hatakiwi kujifanya hafahamiani naye, maana aliwahi kumpa hifadhi nyumbani kwake huko huko Uingereza baada ya Promota wake anayefahamika kwa jina la MUJUNGU kumtelekeza na kushindwa kulipia madeni na Bill zote za hoteli aliyofikia jijini London

 

 

Facebook Comments

Related posts