UTATA WAIGUBIKA RWANDA, NI BAADA YA KUTOWEKA KWA KIONGOZI WA UPINZANI.

Hofu na wasiwasi imekumba jamaa marafiki na chama cha upinzani cha Victoire Ingabire, FDU nchini Rwanda 🇷🇼 baada ya serikali kutangaza kuwa naibu rais wa chama hicho Boniface Twagirimana ametoweka kutoka gereza la Mpanga.
FDU inapinga ripoti ya idara ya Magereza ya Rwanda ikidai haiwezekani mfungwa aliyehamishwa katika gereza hilo lenye ulinzi mkali siku 3 zilizotangulia kutoroka. Boniface ni naibu wa Victoire Ingabire aliyepewa msamaha wa rais Paul Kagame majuzi.

Facebook Comments

Related posts