ZARI kakutana na “Mabango Kama Yote !!” …kisa amempost Rais Museveni !!

SIKU ya Leo Nchini Uganda, ni maadhimisho ya Miaka 56 tangu wapate Uhuru wa Nchi yao, hali ambayo imepokelewa na kusherehekewa vizuri na Raia wa Uganda, huku pongezi tele zikimiminwa kwa Serikali ya Uganda kwa kufikisha miaka hiyo waki Huru bila kutawaliwa na Nchi au mataifa mengine.

Bobi Wine ni moja kati ya watu ambao walitazamwa sana katika kufahamu ni kipi ambacho atakipost ama atakizungumza kuhusiana na Maadhimisho hayo ambaye naye hakusita kuandika katika ukurasa wake wa Instagram kuhamasisha vijana na kizazi cha sasa hivi, kutafuta njia mbadala hasa baada ya viongozi waliopo “kuwapotezea” katika masuala yao Muhimu

Zari The Boss Lady, Mzazi mwenzake na Diamond Platnumz ambaye pia ni mzaliwa wa Uganda, hakuwa nyuma kutoa Salamu za Heri kwa Wakazi wote wa nchi ya Uganda katika maadhimisho ya Uhuru wao tangu 09 OCTOBER 1962 mpaka hivi sasa

kupitia Twitter account yake Zari alipost Picha ya Rais Wa Uganda katika kipindi hiki, YOWERI MUSEVENI kisha akaandika

“Heri ya Uhuru Uganda yangu Pendwa”

Tweet hiyo ambayo ilipata takriban Re-Tweets  36, Zari alishambuliwa na baadhi ya Raia wa Uganda kwa kitendo cha kupost Picha ya Rais Museveni akimpa thamani ya kwamba yeye ndiye Uganda badala ya kupost angalau Bendera ya Taifa hilo.

Katika Tweet hiyo, pia wengine walkionekana kumshangaa sana Mrembo huyo kwa kushindwa kutofautisha mtu binafsi na Nchi ya Ugnada, maana wanaamini kuwa Rais Museveni ni “Mtu” na Uganda ni “Nchi”.

Wengine walifikia mpaka hatua ya kudai kuwa, Zari ameamua kujikita na kukisifia chama tawala cha Rais Museveni kitu ambacho kinatokana na yeye kupewa Ubalozi katika Sekta ya Utalii Nchini Uganda,

Tweet Hizo ni kama Ifuatavyo

Facebook Comments

Related posts