CHEMICAL : “Nilianza KUIMBA kabla ya KU-RAP”

KUPITIA Mkwaju wake wa “Sielewi” wengi tulibaini kipaji kingine cha Ku-rap kutoka kwa Binti ambaye alikuja vizuri na kila mtu kumpokea katika Mtanzamo Chanya kabisa..na hapa tunamzungumzia CHEMICAL  a.k.a “mwana wa Lubao” ambaye bado anazidi kupambana kuhakikisha kuwa jina lake na kazi zake zinaendelea kuwa katika platform nzturi

Hivi sasa Chemical anafanya vizuri sana na mkwaju wake mpya ambao umepewa jina la TILALILA huku humo ndani akionekana kubadilika katika style yake ya ku-rap ambayo wengi tumeizoea kwa asilimia kubwa, yaani humo ndani ameimba, kitu ambacho wengi hawakutarajia kama kweli Chemical huyu huyu anaweza kuwa na sauti tamu kama ile

Akifafanua kuhusu kubadilika kwake na kuja katika mfumo tofauti kabisa, Chemical amesema kuwa, ni kwa sababu ya wengi kutokufahamu kuwa kipindi cha nyuma alikuwa anaimba kabla hata ya kurap

Pia Chemical ameongeza kuwa, aliamua kufanya Rap imtambulishe baada ya kuona kulikuwa na uhitaji wa Rappers wa kike na hawakuwepo wengi, na ndio maana hata alipoanza na Rap, kila mtu alimpokea Vizuri

MSIKILIZE

VIDEO yake ya Tilalila ambayo aliiachia Rasmi Mwezi September katika channel yake ya Youtube, hivi sasa imefikisha Views 148,956. Unaweza kuitizama pia kupitia Hapa :

Facebook Comments

Related posts