Essien umwambii kitu kuhusu Mane.

Mchezaji wa zamani wa Ghana na klabu ya Chelsea, Michael Essien amemtaja nyota wa klabu ya Liverpool Sadio Mane kuwa Mchezaji bora zaidi kwa Bara la Afrika kwa sasa.

Mane (25) amekuwa mmoja wa wachezaji bora Kabisa Katika kikosi cha vijogoo Liverpool.

Mwaka uliopita Mane alikuwa wa pili nyuma ya Mo Salah Katika tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika wa Mwaka.

“Nafikiri Mane alikuwa Vizuri msimu uliopita na msimu huu pia anafanya vizuri hivyo nipo upande wake” maneno ya Essien hayo Katika Mahojiano.

 

Facebook Comments

Related posts