#RIPPanchoLatino : VANESSA MDEE – “Utaishi Milele Katika Muziki”

VANESSA MDEE ni moja kati ya wasanii wengi waliopitia katika Mikono ya Producer Pancho Latino ambaye Hatuko naye tena katika Ulimwengu huu, pigo kubwa ambalo tasnia ya muziki imelipata mpaka hivi sasa

Akiwa bado chini ya B-HITZ pamoja na wasanii wenzake kadha wa kadha akiwemo Mabeste, M-Rap Lion, Deddy, Gosby na wengineo, Vanessa anakiri kuwa alipata vitu vingi vya kujifunza kutoka kwa Marehemu Pancho Latino “Latino Mafia” na bado atabaki navyo hasa akizidi kujivunia kuvifahamu

Ukiachilia mbali kufanya naye kazi tu, Vanessa na Pancho Latino walikuwa ni marafiki wazuri ambapo pia Combination yao katika Kazi, ilikuwa ina nguvu kubwa na production yao ilikuwa ni nzuri kiasi kwamba kila mmoja alikwa akijivunia kusikiliza kazi za wawili hao

Hata kipindi inatangazwa Rasmi kuwa, Familia ya B-Hitz ambayo pia Vanessa alikuwemo inavunjika, wengi waliumia sana maana familia yote kiujumla ilikuwa inaumuhimu mkubwa na ladha yake hasa pale ambapo Pancho latino alikuwa akitia mkono wake katika Kazi zao

Kupitia Instagram account kae, Vanessa Mdee amemuombea Marehemu Pancho Pumziko jema na akaongeza kuwa bado ataendelea kuishi katika Muziki

“Eh Mungu … 😭 Rest Easy Young Legend @pancholatino Thankyou for everything you taught me, you raised me #BHitz you will live forever in the music 🙏🏾. Poleni Sana kwa familia nzima ya #BHitz #LatinoMafia @hermyb pigo kubwa kwenye tasnia ya mziki.”

Jumanne ya September 09, tulipataa taarifa kuwa Pancho hatuko naye tena, ikiwa ni baada ya kuzama katika ufukwe wa Bahari ya Hindi wakati akiogelea  eneo la Kisiwa cha Mbudya,.

Kisiwa cha Mbudya ambako Mauti yalimkuta Pancho Latino, ni sehemu ambayo wasanii wengi sana hupenda kwenda kupumzika na hata kustarehe, huku wengine wakipenda kwenda kufanya Videos mbali mbali wakiwa na Boti kadha wa kadha

Mungu ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi ….Amen

Hii ni Moja kati ya Kazi ambayo Pancho Latino aliitendea Haki ambao familia nzima ya B Hitz ilihusika ndani yake

Facebook Comments

Related posts