Diawara “sijawahi hitaji kuitumikia Italia”.

Kiungo wa Napoli, Amadou Diawara amekanusha Taarifa za yeye kukata wito wa kuchezea Taifa la Guinea Mara kadhaa kutokana na kuwa na matumaini ya kuitwa kuitumikia Italia.

Nyota huyo mwenye miaka 21 ambaye alizaliwa mjini Conakry, kwa sasa yuko Katika maandalizi ya kuitumikia Guinea kwenye Mchezo dhidi ya Rwanda Ijumaa kwenye michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2019.

Kiungo huyo aliweka wazi utayari wake kuitumikia Guinea mapema mwaka huu lakini ikashindikana kucheza kutokana na majeraha ila kwa sasa yuko fiti na atakuwa kwenye kikosi sambamba na Nyota wa Liverpool Naby Keita.

“Imekuwa ni ndoto yangu kuichezea Guinea kwa muda mrefu, sijawahi tamka nitaichezea Italia” maneno ya Diawara.

“Naimani Guinea itapanda kiwango kutokana na kuwa na wachezaji wazuri Mimi pia nitajitahidi kufanya kitu kwenye kikosi “.

Facebook Comments

Related posts