Tamko la Jeshi la polisi Kuhusu kutekwa kwa Dewji.

Taarifa kubwa Katika tasnia ya kandanda leo ni Kuhusu kutekwa kwa Mfanyabiashara mkubwa hapa Tanzania ambaye pia ni muwekezaji mkuu wa Klabu ya Simba Mo Dewji.

Taarifa hizo zimejiri asubuhi ya leo ambapo Mfanyabiashara huyo alikuwa akiingia Katika moja ya Hotel Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi na kutekwa na watu wasiojulikana.

Mpaka hivi sasa hajapatikana na tayari kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa amethibitisha kwamba kwenye Meza yake bado hakuna taarifa za Mo Dewji kupatikana. 

Klabu ya Simba kupitia Afisa habari Haji Manara wameomba wanachama na mashabiki wa Klabu hiyo kuwa watulivu Wakati huu ambao uchunguzi unafanyika ili kupatikana kwa Mo.

Facebook Comments

Related posts