MAMBO 3 KUHUSU ZIARA YA KANYE WEST NCHINI UGANDA-BOBI WINE Kachefukwa…….!!!!

UAMUZI wa Rapper wa kimataifa, KANYE WEST na Mkewe KIM KARDASHIAN kwenda kutembea Nchini Uganda huku sehemu ya dhamira yake kuwepo katika nchi hiyo ikiwa ni Kukamilisha Album yake, umekuwa na mambo mengi sana kiasi kwamba kila kukicha, lazima liibuke jambo Jipya

Ingawa Raia wengi wa Uganda walionekana kufurahiwa na uwepo wake nchini humo, bado kuna baadhi ya vitu ambavyo vilijitokeza, na kama haukufahamu, basi inabidi uchukue nafasi yako kuvifahamu hapa. Ukiachilia mbali kuahidi kutoa misaada katika baadhi ya maeneo ambayo yana uhitaji mkubwa, yafuatayo ni mambo matatu ambayo unatakiwa ufahamu pia.

1.RAIS MUSEVENI ALIULIZA KAZI ANAYOFANYA KIM KARDASHIAN

BAADA ya kuwasili Nchini Uganda, Kanye West na Kim Kardashian walipata nafasi ya kumtembelea Rais wa Nchi hiyo, Yoweri Museven, kitu ambacho kilionekana kuzungumziwa kwa njia hasi na chanya na raia wengi wa Uganda ukizingatia baadhi hawakubaliani na utawala wake.

Baada ya kuonana naye, walimtunuku viatu aina ya YEEZY ambavyo huwa ni Brand ya Rapper huyo ambaye hivi sasa ni sehemu kubwa ya Trend Ulimwenguni kote

Kilichokuja kushtua wengi zaidi, ni baada ya Rais Museveni kuhoji kazi ambayo anaifanya Kim Kardashian, na Kim akamjibu kwa upole na heshima kuwa yeye ni Reality Tv Star na mara baada ya kutoka Nchini humo wataenda kuendeleza Kipindi chao ambacho kinaitwa KEEPING UP WITH THE KARDASHIANS

Kwanini hiyo ilionekana kuwa Stori kubwa, ni baada ya wengi kujiuliza kuwa, inakuaje Rais Museveni anapokea wageni/Mgeni ambaye hafahamu anajishughulisha na nini, na hicho kitu anachojishughulisha nacho kina umuhimu gani katika maisha yake, ili kama kinafaa, basi aandae hata mazingira ya kuwaunganisha watu wengi wa Uganda ambao pengine wanapenda ama wanafanya kitu kama anachokifanya mgeni wake

2. BOBI WINE KACHEFUKWA KUHUSU KANYE WEST

Msanii Bobi Wine ambaye pia ni Mbunge wa wa jimba la Kyaddondo Mashariki, alifurahishwa pia na uwepo wa Kanye West na Kim Kardashian West kuwepo Nchini Uganda ukizingatia amekuwa akijitahidi kuhakikisha vijana wenye vipaji na hata mawazo ya biashara wakifanya shughuli zao na kuepukana na maisha ya hali ya chini

Lakini kama Mwanaharakati ambaye anapinga kabisa unyanyasaji na uonevu wa Serikali hasa kwa vijana ambao wanapambania uhuru na amani yao katika nchi ya Uganda, hakufurahishwa na kitendo cha Msanii huyo kwenda kukutana na Rais Museveni ambaye anaamini anakumbatia sana Uonevu katika Haki na Uhuru wa Kuzungumza hadharani

Bobi Wine anadai kuwa Kitendo alichokifanya kumtembelea Rais ambaye yupo madarakani kwa Miaka 32 na bado haruhusu kuwepo na uhuru wa maoni hasa kwa vijana, ni kulidhalilisha jina lake kubwa Duniani, badala yake angeungana na Waganda wengi ambao wanaumizwa na Rais huyo kupiga kile anachokifanya.

“Sio Busara kwake. Kumtembelea na kuonekana kufurahia na Rais ambaye amekuwa madarakani kwa Miaka 32 akizuia Uhuru, Nchi ambayo wanaharakati wanakamatwa na kufungwa” alisema Bobi Wine

3. ETI KANYE WEST ALIISHIWA MKWANJA

SIKU zote visa huwa havikosekani , hata kama utakuwa umefanya jambo jema na kufuata Ratiba zako.  Wengi walitarajia kuwa Kanye West angekaa Uganda muda mrefu kutokana na kazi ambazo aliahidi kuzifanya. Lakini ghafla ilitolewa taarifa na Waziri wa Utalii Nchini Uganda, Godfrey Kiwanda kuwa Kany West na Mkewe watasafiri haraka sana kurudi Nchini Marekani kwa ajili ya kukamilisha mipango ya kufanya nao kazi katika Sekta ya Utalii.

Kama unavyojua, Waungwana waliamua kutoa madongo kunako mitandao ya kijamii kuwa Kanye huenda kaishiwa kutokana na gharama za Hoteli aliyofikia kuwa juu zaidi. Lodge hiyo ambayo huwa inaogopwa sana kwa gharama zake, inaitwa SAFARI LODGE, hivyo wengi walianza kutuhumu kuwa huenda Kanye West alihisi kabisa kuwa mkwanja wake hautoshi, hivyo bora asepe mapema

 

Facebook Comments

Related posts