Shaw ajipiga kitanzi Old Trafford cha miaka mitano.

Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw amejitia kitanzi Old Trafford Baada ya kusaini mkataba mpya kwenye Klabu hiyo ambapo atakuwa anapokea kitita cha £ 190000 Sawa na $250000 Manchester United wamekubaliana kuafikiana na mchezaji huyo Katika mkataba wake mpya ambao unamfanya kuwa mmoja wa mabeki wanaolipwa vizuri nchini England. Baada ya taarifa hiyo kutolewa Shaw ameapa kupigana kufa na kupona kuonyesha kile ambacho mashabiki wanahitaji Katika miaka ijayo. “Mi Bado mdogo kuna vitu vingi vya kujifunza siwezi kungoja kuendeleza kipaji changu chini ya Jose Mourinho” Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

AMUUA MWANAFUNZI MWENZAKE KWA KISU MBELE YA WANAFUNZI WENZAKE NI KWA DENI LA SHILINGI MIA SITA

  Mwanafunzi mmoja wa Kidato cha Pili katika Shule ya Upili ya Lugusi Boys Secondary Kaunti ya Kakamega nchini Kenya amejikuta katika mikono ya polisi Malava baada ya kutuhumiwa kumdunga kisu mwenzake na kusababisha kifo kwa deni la shilingi mia sita za Kenya. Mwanafunzi huyo ambaye jina lake halikutajwa inadaiwa alimchukua mwenzake na kwenda kwa mdeni wao na kumlazimisha awalipe fedha hizo kisha kumdunga kisu hicho baada ya kuwaeleza kuwa hana fedha hizo na kuzuka majibizano . Kulingana na ripoti za kuaminika kutoka Kakamega, kisa hicho kilitokea shuleni na kilishuhudiwa…

Facebook Comments

Read More

KESI YA MWALIMU WA POPOBAWA KUMLAWITI MWANAFUNZI WAKE ARUSHA MAMBO BADO

  Mahakama katika mkoa wa Arusha imeuagiza upande wa mashtaka kuhakikisha unamleta shahidi wa kesi ya ulawiti inayomkabili mwalimu wa shule ya sekondari Adili ya mkoani humo anayedaiwa kufanya kisa hicho kwa mwanafunzi wake wa kiume. Hakimu anayesikiliza kesi hiyo hakimu mkazi Patricia Kisinda amefikia uamuzi huo kufuatia kutoonekana mahakamani hapo zaidi ya mara mbili kwa shahidi huyo ambaye ni daktari aliyemfanyia vipimo mwanafunzi huyo kabla ya kuahirisha kesi hiyo hadi October 28 mwaka huu . Awali muendesha mashtaka wa serikali Naomi Mollel aliieleza mahakama kuwa shahidi ameshindwa kutokea kwa…

Facebook Comments

Read More

MAJERUHI KUMI NA NNE WA RADI GEITA WARUHUSIWA

Wanafunzi kumi na nne kati ya ishirini na moja wa shule ya msingi Emarco Vision waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Geita baada ya kujeruhiwa na radi wameruhusiwa kutoka hospitali. Wanafunzi hao ni wale waliokumbwa na tukio la radi lilitotokea juma tano October 17 2018 wakati wanafunzi hao wakiwa darasani. Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Moses Simon alisema wanafunzi wengi waliathirika maeneo ya miguuni na shingoni. Tayari shughuli za mazishi zinaendelea kufanyika kwa wanafunzi ambao walipoteza maisha katika tukio hilo. Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

Hadi La Pulga anamuhitaji mnyama Pogba Catalunya.

Majira ya kiangazi ofa ya Barcelona ilikataliwa na Manchester United ya kumnasa Paul Pogba , lakini Barcelona wanataka kurejea tena kwasababu wachezaji kadhaa wanamtaka mfaransa huyo kikosini. Taarifa kutoka Hispania zinasema kwamba Wafaransa wenzake Ousmane Dembele na Samuel Umtiti wanataka Pogba apeleke kiwango chake cha Kombe la Dunia Nou Camp. Lakini pia  Lionel Messi na Gerard Pique nao wameonesha nia ya kutaka kumuona Pogba Catalan. Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

KAMATI KUU CHADEMA YAWACHUKULIA HATUA KUBENEA NA MWENZAKE

Kamati Kuu ya Chadema, imewavua nafasi zote za Uongozi na kuwaweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, Saed Kubenea na Anthony Komu baada ya kukiri kusambaza sauti iliyolenga kudhohofisha chama. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika amesema, katika uamuzi huo wa Kamati Kuu, wabunge hao wamekiri makosa yao katika mkutano walioitwa mbele ya kamati na kuomba radhi kama walivyotakiwa kufanya. Kwa mujibu wa Mnyika, wabunge hao pia wamevuliwa nyazifa zao ndani ya chama na kuwekwa chini ya uangalizi kwa miezi 12. Facebook Comments

Facebook Comments

Read More

Jinamizi la kuondokewa na King James limeanza kuitafuna Cavaliers wanyukwa na Raptors.

Msimu mpya wa ligi ya Basketball nchini Marekani (NBA)  Umeingia siku ya pili kwa Michezo kadha wa kadha kupigwa. Alfajiri ya leo mambo hayakuwa mazuri kwa makamu Bingwa Cleveland Cavaliers Baada ya kucharazwa kwa points 116 kwa 104 dhidi ya Raptors. Cavaliers imeondokewa na Star wake Lebron James ambaye alihamia Lakers kitu ambacho kinsemekana huenda wakawa Katika hali ngumu msimu huu. Katika mchezo huo ulipigwa pale Katika uwanja wa Scotiabank nyumbani kwa Raptors wachezaji waliyeonekana mwiba kwa Cavaliers ni Kawhi Leonard na Kyle Lowry ambao Wote kwa pamoja walipachika points…

Facebook Comments

Read More