KAMATI KUU CHADEMA YAWACHUKULIA HATUA KUBENEA NA MWENZAKE

Kamati Kuu ya Chadema, imewavua nafasi zote za Uongozi na kuwaweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, Saed Kubenea na Anthony Komu baada ya kukiri kusambaza sauti iliyolenga kudhohofisha chama.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika amesema, katika uamuzi huo wa Kamati Kuu, wabunge hao wamekiri makosa yao katika mkutano walioitwa mbele ya kamati na kuomba radhi kama walivyotakiwa kufanya.

Kwa mujibu wa Mnyika, wabunge hao pia wamevuliwa nyazifa zao ndani ya chama na kuwekwa chini ya uangalizi kwa miezi 12.

Facebook Comments

Related posts