Shaw ajipiga kitanzi Old Trafford cha miaka mitano.

Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw amejitia kitanzi Old Trafford Baada ya kusaini mkataba mpya kwenye Klabu hiyo ambapo atakuwa anapokea kitita cha £ 190000 Sawa na $250000

Manchester United wamekubaliana kuafikiana na mchezaji huyo Katika mkataba wake mpya ambao unamfanya kuwa mmoja wa mabeki wanaolipwa vizuri nchini England.

Baada ya taarifa hiyo kutolewa Shaw ameapa kupigana kufa na kupona kuonyesha kile ambacho mashabiki wanahitaji Katika miaka ijayo.

“Mi Bado mdogo kuna vitu vingi vya kujifunza siwezi kungoja kuendeleza kipaji changu chini ya Jose Mourinho”

Facebook Comments

Related posts