#KamataMwizi : Kundi la THE MIGOS Wanashtakiwa kwa Kuiba wimbo “WALK IT TALK IT”

HAKIKA kila mtu ambaye anafuatilia Muziki wa HIP HOP duniani kote, basi atakuwa anaufahamu fika kabisa mkwaju wa Kundi la MIGOS “Walk It Talk It” ambao ulionekana na bado unaendelea kupendwa na kukubalika kupita maelezo

Lakini  kwa bahati mbaya, Mkwaju huo umesababisha kundi la Migos ambao walimshirikisha Rapper Drake, wafunguliwe mashtaka na msanii kutoka ATLANTA anayefahamika kwa jina la M.O.S ambaye amedai kuwa kundi hilo limeiba wimbo wake na kuufanya kuwa wa kwao

Rapper M.O.S amedai kuwa , Wimbo wa “Walk It Talk It ” kutoka kwa Kundi la Migos, umechukuliwa baadhi ya vitu kutoka katika Wimbo wake unaoitwa “WALK IT I TALK IT” na alimshirikisha msanii mwenzake B-$TACK$. Pia wimbo huo unatoka katika Mixtape ya  “It’s Like a Movie,” ambayo iliachiwa rasmi na  M.O.S pamoja na DJ Folk.

Katika malalamiko yake, M.O.S ambaye jina lake halisi ni Leander Pickett anafafanua kuwa wimbo huo uliachiwa rasmi Mwaka 2007 na kupata hakimiliki yake mwaka 2018, hivyo kitendo walichokifanya MIGOS, ni kinyume na haki zake za msingi na wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria

HEBU chukua “time” yako kusikiliza Nyimbo zote halafu utatoa maoni yako

  1. THE MIGOS FEAT. DRAKE – WALK IT TALK IT

    2. M.O.S FEAT B-$TACK$- WALK IT I TALK IT

Facebook Comments

Related posts