Lopetegui rasmi atimuliwa Madrid baada ya kuingoza kwenye mechi 14 tu.

Hatimaye Klabu ya Real Madrid imemfungashia virago aliyekuwa kocha wake Julen Lopotegui baada ya kuingoza Madrid kwa takribani mechi 14, na hili limejiri Baada ya kupokea kisago cha goli 5-1 toka kwa Barca wikendi iliyopita. Santiago Solar ambaye alikuwa akipendekezwa kurithi mikoba ya Lopotegui kwa muda, sasa amepewa nafasi hiyo. Real Madrid wameshindwa kupata ushindi kwenye LA Liga tangu wamfunge Espanyol September 22 baada ya hapo wakapoteza dhidi ya Sevilla,  Alaves, Levante na kutoka sare na Atletico Madrid kabla ya Kipigo kizito cha goli 5-1 toka kwa Barca. Lopotegui mwenye…

Read More

WANAOSAMBAZA VIDEO NA PICHA ZA NGONO KUKIONA

  Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imeapa kula sahani moja na wale wote wanaosambaza video au picha za ngono katika mitandao ya kijamii. Mamlaka hiyo imesisitiza kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kutenda makosa hayo. Hatua hii inakuja ikiwa ni siku chache tangu kusambaa kwa video ya msanii Wema Sepetu pamoja na ya binti mwingine maarufu kwa jina la Amber rutty zenye maudhui ya ngono.

Read More

GAZETI LA TANZANITE KITANZINI, NI BAADA YA KUANDIKA HABARI ZILIZOZUA UTATA

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema habari iliyochapishwa na gazeti la kila siku la Tanzanite la leo Jumatatu tarehe 29 Oktoba, 2018 lenye habari zenye tuhuma za kisiasa dhidi ya Viongozi kadhaa, haziakisi msimamo wa Serikali na ameagiza mmiliki na Bodi ya uhariri ya gazeti hilo waitwe mara moja Idara ya Habari (MAELEZO) kujieleza kuhusu msingi wa habari hiyo. Dkt. Mwakyembe ametoa ufafanuzi huo leo mchana, mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuelezea kushtushwa kwake na…

Read More

Ajali ya Helicopter Mbali na kumchukua mmiliki wa Leicester City imeondoka na Mrembo.

Baada ya kuthibitishwa kifo cha bilionea wa Kithailand na mmiliki wa Klabu ya Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha ambae alifariki kutokana na ajali ya Helicopter iliyotekea Jumamosi nje ya uwanja wa King Power Stadium waliofariki wengine wametambulika. Mmoja Wapo wa waliofariki ni Mrembo Nusara Sukinamai ambaye alishawahi kushiriki mashindano ya Miss Thailand Universe. Baadhi ya wadau wametoa salamu zao za rambirambi kuhusu kifo Cha Vichai ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Leicester City. “Ulikuwa mtu wa kufariji Kila mtu pasipo wezekana kuwezekana” Maneno ya kipa wa Leicester City,  Schmeichel.

Read More

Ajibu na Tshishimbi kwenye hatihati kuwavaa Lipuli Kesho.

Kikosi cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake Asubuhi ya leo Kuelekea Katika mchezo Wao wa Kesho wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Lipuli utakao pigwa Katika uwanja wa Taifa. Meneja wa Klabu Yanga beki na nahodha wa zamani wa Klabu hiyo Nadir Haroub Canavaro ameweka wazi kuwa maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vyema. Kuhusu Tshishimbi na Ajibu hali zao zinaendelea vizuri lakini bado haijulikana kwamba watakuwa Sawa kwa mchezo wao Kesho. Yanga inashuka dimbani Kesho ikiwa mpaka sasa hawajapoteza mchezo wowote Katka ligi wakishika nafasi ya tatu…

Read More

MWALIMU ANASWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE OFISINI 

Mwalimu mmoja wa shule ya msingi katika eneo la Njoro, kaunti ya Nakuru anazuiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake kwenye ofisi ya walimu.  Mwalimu huyo anadaiwa alimuita mwanafunzi huyo katika ofisi na kisha kumlazimisha kufanya naye mapenzi ikiwa ni siku chache kabla ya mwanafunzi huyo kuanza mtihani wa darasa la nane. Mwanafunzi huyo alikubali na wakaanza kutekeleza tukio hilo kabla ya mwalimu mmoja kushtukia na kutoa taarifa kwa uongozi ambao walifika na kufanikiwa kuwanasa wakiendelea na tukio hilo. Naibu wa chifu eneo hilo alithibitisha kuwa mwalimu huyo…

Read More

Hamilton katuma salamu za Shukran kwa waliomsapoti mpaka kuwa bingwa Formula 1 mwaka 2018.

Bingwa wa Dunia wa michuano ya Formula One Lewis Hamilton ameahidi kufanya makubwa kwa timu yake ya Mercedes nakuifanikisha kubeba mataji. Kupitia mtandao wa Twitter Lewis Hamilton ameweka video akiwashukuru waliomuunga mkono mpaka anakuwa Bingwa ikiwemo timu yake na akaeleza anaelekea Los Angeles akiwa na matumaini yakuwaona Mbwa wake na Kisha anarejea ulaya kukutana na timu. Lewis Hamilton Jana alishika nafasi ya nne Katika mbio za Mexican GP na kufanikiwa kuchukua taji la Dunia la Formula One 2018. Katika mbio hizo za Mexico Dereva wa Red Bull,  Max Verstappen alishika…

Read More