Lopetegui rasmi atimuliwa Madrid baada ya kuingoza kwenye mechi 14 tu.

Hatimaye Klabu ya Real Madrid imemfungashia virago aliyekuwa kocha wake Julen Lopotegui baada ya kuingoza Madrid kwa takribani mechi 14, na hili limejiri Baada ya kupokea kisago cha goli 5-1 toka kwa Barca wikendi iliyopita.

Santiago Solar ambaye alikuwa akipendekezwa kurithi mikoba ya Lopotegui kwa muda, sasa amepewa nafasi hiyo.

Real Madrid wameshindwa kupata ushindi kwenye LA Liga tangu wamfunge Espanyol September 22 baada ya hapo wakapoteza dhidi ya Sevilla,  Alaves, Levante na kutoka sare na Atletico Madrid kabla ya Kipigo kizito cha goli 5-1 toka kwa Barca.

Lopotegui mwenye umri wa miaka 52 rasmi sasa kapoteza kazi mbili ndani ya kipindi cha chini ya miezi mitano.

Ikumbukwe alifukuzwa kama kocha wa Spain siku moja kabla ya Michuano ya kombe la Dunia kuanza mwezi, wakati akiandaa mipango ya Kuhamia Bernabeu bila ya kushirikisha chama cha soka Spain.

Related posts