Besiktas hichi ndicho wanachotaka kumfanyia Karius.

Zimetoka taarifa kuwa Klabu ya Besiktas ya Uturuki ipo mbioni kuukatisha mkataba wa mkopo wa Loris Karius ili mlinda mlango huyo arejee kwenye Klabu yake ya Liverpool.

 

Kwa Mara ya kwanza Karius amekaa langoni kuidakia Besiktas ni Katika mechi dhidi ya Bursaspor iliyomalizika kwa sare ya 1-1 mchezo ulipigwa Sept 2.

Tangu hapo Karius amekaa kwa ujumla mara 11 akiruhusu nyavu zake kuguswa mara 16, akiwa ameisaidia timu yake kushinda michezo mitano akiwa langoni na wakitoka sare 3 na timu kufngwa mara yeye akiwa langoni.

Mkataba wa mkopo wa Loris Karius Katika klabu ya Besiktas unamalizika kwenye majira ya kiangazi 2020.

Related posts