Kiwango cha Barkley chamkuna Carragher.

Nyota wa Klabu ya Chelsea anayekuja juu hivi Sasa Ross Barkley anaweza kuwa muhimili mkubwa Katika kikosi cha Timu ya taifa ya England chini ya kocha Gareth Southgate kwa mujibu wa mlinzi wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher.

Kiungo huyo wa Chelsea alifanikiwa kucheka na nyavu wikendi iliyopita ikiwa ni katika michezo mitatu mfululizo kufanya hivyo na Carragher anaamini nyota huyo wa zamani wa Everton ataonyesha ubora huo pia Katika taifa.

Ukifananisha uwezo wa sasa wa Barkley na alivyokuwa Everton, Carragher anadai uwezo wamchezaji huyo umekuwa zaidi kwa sasa.

Related posts