FAINALI YA KLABU BINGWA AMERICA YA KUSINI KUCHEZWA MADRID RAISI (CONMEBOL) AWATAKA MASHABIKI WAJIHESHIMU.

Raisi wa shirikisho la kandanda Amerika ya kusini (CONMEBOL)  Alejandro Domiguez amewataka Mashabiki kujieheshimu Kuelekea fainali ya pili ya (COPA LIBERTADORES) michuano ya Klabu bingwa barani America ya kusini unapangwa kupigwa jijini Madrid. Boca Juniors na River Plate wataumana katika Uwanja wa Santiago Bernabeu siku ya December 9 kumalizia mechi ya marudiano ambapo mechi ya mwanzo ilimalizika kwa sare ya 2-2. Mchezo huo awali ulikuwa uchezwe nyumbani kwa River Plate pale El Monumental lakini mechi ikaahirishwa baada ya basi la Boca kuvamiwa njiani likielekea wa uwanjani. Sasa mchezo huo utachezwa…

Read More

BEKI HILI KUTOKA IVORY COAST LATUA RASMI MSIMBAZI.

Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba wamethitisha kunasa saini beki wa kushoto kutoka Ivory Coast ajulikanaye kama Zana Coulbaly.   Taarifa kupitia ukurasa wa Instagram wa Simba imesomeka “Tunapenda kuwatangazia kwamba beki Zana Coulibaly kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast leo atawasili nchini kwa ajili kukamilisha taratibu za mwisho kujiunga na timu yetu ili kuziba pengo la beki Shomari Kapombe ambaye siku za karibuni alipata majeraha. #SSC #NguvuMoja” Simba ni Klabu ambayo ina michuano mingi yakushiriki msimu huu ikiwemo michuano ya Klabu bingwa barani Afrika hivyo kinahitajika kikosi kipana cha…

Read More

Hatimaye aliyeshambulia basi la Dortmund kwa bomu mwaka 2017 auhukumiwa miaka 14 Jela.

Hatimaye mtu aliyefanya shambulizi la bomu kwenye basi la kusafiria la Klabu ya Borrusia Dortmund mwaka 2017 amehukumiwa Jela kwa kifungo cha miaka 14 kwa kosa la kujaribu Kufanya mauaji. Mtu huyo ajulikanaye kifupi kama Sergej W. amekutwa tuhuma hiyo na kuhukumiwa leo na mahakama mjini Dortmund. Hata hivyo alitakiwa kulipa kiasi cha euro 15000 kwa beki wa Dortmund Marc Bartra ambaye alipata majeraha kwenye shambulio hilo ambaye alitakiwa kufanyiwa upasuaji kutoa vipande vya kioo vilivyo ingia mkononi. Askari mmoja pia alijeruhiwa katika shambulio hilo ambapo milipuko mitatu ililipukia basi…

Read More

Majeruhi yaiandama City Kocha achagua jembe lake kuimaliza Lyon Leo.

Usiku wa Ulaya, michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya imerejea na ipo katika hatua ya makundi leo jumanne na kesho jumatano pia kuna michezo inapigwa. Kuelekea michuano hii Kocha wa Manchester City amependekeza kumtumia kinda Phil Foden Kwamba ataanza katika mchezo ambao wataumana na Lyon ya Ufaransa. City wanaingia katika mchezo wa leo pale katika dimba la Groupama bila ya Nyota wao kadhaa kama Bernado Silva na Ilkay Gundogan. Bwana mdogo Foden amecheza kwa dakika 3 tu msimu huu kwenye michuano ya Klabu bingwa barani Ulaya lakini ametokea bechi Mara…

Read More

Baada ya kuandamwa na Maneno dogo afikia maamuzi haya, huwezi amini.

Ousmane Dembele ameiomba Klabu Barcelona imruhusu aondeke katika dirisha la usajili Mwezi January taarifa hii inachangiza uvumi kutoka vyanzo mbalimbali vya habari kuhusu kurejea kwa Neymar Camp Nou. Dembele ameshindwa kuendana na mfumo wa Barcelona tangu ajiunge na Klabu hiyo ya pale Catalunya mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmund kwa dau la paundi milion 93 Sawa na Euro milioni 105 na sasa anaomba uongozi wa Barcelona umfungulie mlango aondoke. Taarifa zinadai Barcelona iliyopo chini ya Kocha Ernesto Valverde inajipanga kumjumuisha Dembele kwenye dili litakalomng’oa Neymar pale Paris nakurejea Catalunya. Vilabu vya…

Read More

Hazard awakatalia mchana kweupe matajiri wa Jiji la Paris wasijisumbue kumtafuta.

Nyota wa klabu ya Chelsea Eden Hazard hakubaliani na mipango ya kuhamia Paris Saint-Germain lakini amekumbushia kwa inawezekana kuhama darajani. Eden Hazard amekuwa akihusishwa kuhama darajani kitambo ikiwa ni kabla na baada ya kombe la Dunia na kujiunga hasa na Real Madrid. Hazard mwenyewe alishaonyesha hamu yake ya kutaka kujiunga na matajiri wa jiji la Madrid ( Los Blancos) lakini hata hivyo Chelsea wamekuwa wakipambana kuhakikisha Nyota wao huyo haondoki kizembe. Lakini Hazard akiwa katika mahojiano na wanahabari Hazard alikubali kuhusu taarifa za yeye kuwindwa na Paris Saint-Germain inayoshiriki Ligue…

Read More

AMUUA MKEWE KWA PANGA,NI BAADA YA KUMFUMANIA NA MWANAUME MWINGINE CHUMBANI KWAKE

  Mwanaume mmoja Paul Maritim ameripotiwa kumuua mkewe kwa kumchinja shingoni kwa panga baada ya kumkuta akifanya mapenzi na mwanaume mwingine chumbani kwao. Mbali na mauaji hayo pia mwanaume huyo mkazi wa kijiji cha Kapregerego kaunti ya Nakuru nchini Kenya anadaiwa kumjeruhi kwa mapanga mwanaume aliyemfumania na mkewe wakifanya tendo hilo. Siku ya tukio Maritimu alirejea nyumbani kwake na kumfumania mkewe akiwa na mwanaume chumbani kwake jambo lilimghadhabisha na kuamua kuchukua panga na kuwashambulia. Majirani waliofika katika eneo la tukio kushuhudia kilichokuwa kikiendelea, inasemekana walifurushwa na Maritim huku akitishia kuwakatakata…

Read More

Mane akubali maisha ya kubaki Anfield mpaka 2023

Sadio Mane amekubaliana na klabu yake ya Liverpool kuhusu kupewa mkataba mpya wa muda mrefu katika klabu hiyo, mkataba ambao utamuweka Anfield mpaka mwaka 2023. Kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp amemwagia sifa nyota huyo Msenegal akidai “sidhani kama kuna klabu hata moja Ulaya itakataa kuwa na mchezaji kama yeye”. Mane mwenye umri wa miaka 26 amefunga magoli 40 kwenye michezo 89 aliyoichezea Liverpool tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Southampton kwa dau la paundi milion 34 kwenye majira ya kiangazi mwaka 2016. Mane akizungumzia mkataba wake mpya “nina furaha…

Read More

Zabaleta amkaribisha kwa Mikono miwili Nasri wawe pamoja tena kwa wagonga nyundo.

Kumpata nyota wa zamani wa Arsenal na Manchester City, Samir Nasri kutasaidia kuongezeza kuongeza nguvu kwenye kikosi cha wagonga nyundo wa London Westham United na hilo ni kwa mujibu wa Pablo Zabaleta. Mara ya mwisho Nasri kucheza kwenye mechi ya kimashindano ni takribani mwaka mmoja umepita, akiwa anaitumikia Antalyaspor katika ligi kuu ya soka nchini Uturuki, na sasa anajipanga kurejea uwanjani Tangu atoke kwenye kifungo cha matumizi ya Dawa zisizo ruhusiwa michezoni ambapo tayari ameshapata matibabu katika mji wa Los Angeles mwaka 2016 wakati akiwa kwa mkopo Sevilla.  Adhabu aliyokuwa amepewa…

Read More

AUA MWANAYE KWA MPINI WA JEMBE AKIMTUHUMU KUIBA KUKU.

  Polisi mkoani Manyara wanamshikilia mwanamke mmoja Mariam Daudi kwa tuhuma za kumuua mwanaye kwa madai ya kuiba njiwa wa jirani. Mwanamke huyo mkazi wa Komoto wilaya ya Babati mkoani humo anadaiwa kumuua mwanaye Emanuel Justine (11) mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kwang’w. Kamanda wa polisi mkoani humo Augustino Senga alisema mwanamke huyo siku ya tukio alipokea taarifa kuwa mwanaye aliiba njiwa za jirani. Baada ya kupokea taarifa hizo alimkamata mwanaye kwa kushirikiana na anayedaiwa kuiba njiwa kisha kumfunga kamba mikono na miguu kisha kuanza kumcharaza…

Read More