AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKOJOLEA DUKA LA MKEWE, MWENYEWE ADAI LENGO NI KUMLAANI MKEWE ALIYEMNYIMA CHAKULA

 

Mwanume mmoja Simon Wachira (53) mkazi wa eneo la Mikindani kaunit ya Mombasa nchini Kenya ambaye anatajwa kuwa mlevi wa kupindukia amefikishwa mahakamani kwa kosa la kukojoa mbele ya duka la mkewe.

Mwanume huyo anadaiwa kutenda kisa hicho 23 October mwaka huu kwa lengo la kumlaani mkewe na watoto wake waliokataa kumpa chakula ili hali anjaa kabla ya kufikishwa mahakamani Jumanne 30 October mwaka huu .

Akijitetea mbele ya hakimu mkuu Julius Nange’a, Wachira alikiri kutekeleza kitendo hicho cha aibu na kusema kuwa nia yake ilikuwa ni kumlaani mkewe ambaye ametelekeza majukumu yake kama mke.

Kulingana na Wachira, alighadhabishwa na mkewe kwa kumnyima pesa ilhali duka hilo ni yeye alimfungulia ili waweze kuendesha biashara kwa pamoja.

” Ningependa mahakama inisamehe kwa sababu nilikuwa mlevi wakati nilifanya kitendo hicho, hata sikumbuki vema yale yaote yaliojiri, lakini nilighadhabishwa sana baada ya mke wangu niliyemuoa kihalali pamoja na mwanangu niliyemlipia karo hadi chuo kikuu kusema kwamba hawawezi wakalisha mtu mlevi kama mimi,” Wachira aliiambia mahakama

Facebook Comments

Related posts