ZITO AACHIWA KWA DHAMANA, NI BAADA YA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

 

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe (ACT) ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka matatu ikiwemo kutoa maneno ya uchochezi na kuyakana yote.

Kwa mujibu wa Wakili wake, Jebra Kambole, Zitto ameyakana mashtaka yote matatu na kesi imeahirishwa hadi Novemba 26 mwaka huu.

Masharti ya dhamana ilikuwa ni kuwa na mdhamini mmoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 10.

Facebook Comments

Related posts