Esperance yaanza na kipigo fainali za Klabu bingwa Afrika.

Klabu ya Esperance ya Tunisia imeanza vibaya harakati za kuutafuta ubingwa wa tatu kihistoria Katika michuano ya kombe la Klabu bingwa Afrika baada ya kucharazwa goli 3-1 na Al Ahly ya Misri.

Katika mchezo huo uliopigwa Alexandria nchini Misri umeshuhudia wenyeji Al Ahly wakiimaliza Esperance kwa magoli matatu mwawili yakiwa ya Penalty.

Magoli yakifungwa na Walid Solmani dk ya 34 kwa penati baadae wenyeji wakapata goli la pili kupitia kwa Amr Al Sulaya kabla ya Esperance kupata bao pekee dk ya 65 kupitia kwa Mohamed Youcef kabla ya wenyeji kupigilia msumari wa mwisho kupitia kwa Walid kwa penati nyengine ya dk ya 78.

Mchezo wa Marudiano utakaoamua Mshindi wa michuano hii mwaka 2018 utapigwa tarehe 9 mwezi November kule Tunisia.

Facebook Comments

Related posts