Sarri awapa makavu Drinkwater na Victor Moses kuutafuta mlango wa kutokea.

Danny Drinkwater na Victor Moses wanajipanga kuangalia mlango wa kutokea Katika Klabu ya Chelsea baada ya Maurizio Sarri kufichua wachezaji hao hawaendani na mipango yake.

Kocha huyo wa Chelsea amewambia Nyota hao kwamba waongeze juhudi kama wanahitaji kupata nafasi Katika mfumo wake.

Victor Moses amecheza katika michezo sita tu ya Chelsea Msimu huu Katika michuano yote huku Drinkwater alitokea benchi kwenye Mchezo wa Community Shield wakifungwa na City mwanzoni mwa Mwezi August.

“Wanapaswa kuongeza juhudi lakini sifa zao zipo tofauti kidogo” Sarri.

Facebook Comments

Related posts