Kamati ya maadili ya TFF yamdondoshea rungu zito Kuuli.

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) iliyokutana Jumamosi Novemba 3,2018 imemfungia maisha kutojihusisha na Mpira wa Miguu aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Revocatus Kuuli aliyeshtakiwa katika Kamati hiyo kwa makosa matatu.

Pichani Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Hamidu Mbwezeleni akitoa ufafanuzi wa hukumu hiyo

 

Kuuli amefungiwa kufuatia sakata la uchaguzi Simba ambapo alihojiwa kwanini ameamua kuuzuia mchakato wake kipindi unaanza na kupewa siku tatu kwa ajili ya kutoa majibu.

Wakili huyo alipewa siku hizo na Katibu Mkuu wa Shirikisho, Wilfred Kidao lakini hakuweza kujibu chochote na kisha baadaye kuja na majibu ya dhihaka na lugha kali kwa Kidao.

Hata hivyo, Kuuli baadaye kabla hajafungiwa ilielezwa kuwa angetangaza kuachia nafasi hiyo ndani ya TFF akielezwa kukerwa kuingiliwa kwenye majukumu yake ya kazi.

Licha ya kuuzia mchakato wa uchaguzi Simba, klabu hiyo iliendelea nao kama kawaida ambapo jana rasmi imefanikisha kufanya uchaguzi wake na kuwapata viongozi wapya.

 

 

Facebook Comments

Related posts