Myweather kuja kitofauti mwishoni mwa mwaka pale Japan.

Floyd Mayweather ametangaza atapambana na Tenshin Nasukawa siku ya kuukaribisha mwaka mpya pale Japan.

Myweather Tayari ameshasaini na chama cha promotion cha mchezo wa MMA pale Japan pamoja na shirikisho la mchezo wa MMA Japan liitwalo RIZIN FIGHTING Federation na sasa anajipanga tu kuzichapa na Nasukawa mwenye umri wa miaka 20.

Bingwa huyo wa Dunia Katika wa ndondi Katika mataji matano ya uzito tofauti Myweather hajawahi kupapamba kwenye Mchezo wa MMA.

Katika mkutano na wanahabari mjini Tokyo leo Myweather anasema “nilihitaji kufanya kitu cha tofauti. Nilihitaji kuonyesha uzoefu wangu nje ya U.S. na kuwa Katika Katika pambano la kipekee”

Huku Sheria za Boxing zikiwa haziruhusu matumizi ya mateke lakini kwa upande wa Sheria za MMA zenyewe zinajumuisha mateke, kutumia magoti na viwiko pamoja na mieleka na kukabana viwiko na ukiangalia Myweather ni Boxer tunasubiri kumuona kwenye upande huu.

 

Facebook Comments

Related posts